title : WATAALAM NISHATI, REA, TANESCO WAKAGUA MIRADI YA REA MOROGORO
kiungo : WATAALAM NISHATI, REA, TANESCO WAKAGUA MIRADI YA REA MOROGORO
WATAALAM NISHATI, REA, TANESCO WAKAGUA MIRADI YA REA MOROGORO
Wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wamefanya ziara katika vijiji vya Mandera, Mtego wa Simba na Kibaoni vilivyopo mkoani Morogoro. Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kukagua utekelezaji wa miradi ya usambazaji wa umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) Katika ziara hiyo ilielezwa kuwa, kampuni ya State Grid iliyopewa kazi hiyo katika mkoa wa Morogoro inatarajiwa kuwasha umeme katika vijiji vya Mandera, Mtego wa Simba na Kibaoni tarehe 16 Mei, 2018.
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro, Mhandisi Hassan Saidy (katikati) akielezea hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa miundombinu ya umeme katika kijiji cha Mandera kilichopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro kwa wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika ziara hiyo. Kulia ni Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Yusuph Msembele.
Moja ya transfoma zilizofungwa na kampuni ya State Grid katika kijiji cha Mandera kilichopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
Meneja Mwandamizi wa TANESCO- Kanda ya Kati, Mhandisi Atanasius Nangali ( wa pili kulia) akifafanua jambo katika ziara hiyo.
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro, Mhandisi Hassan Saidy (kushoto) akimsikiliza mwananchi wa kijiji cha Kibaoni kilichopo wilayani Mvomero mkoani Morogoro, Joseph Mkude (kulia) katika ziara hiyo.
Hivyo makala WATAALAM NISHATI, REA, TANESCO WAKAGUA MIRADI YA REA MOROGORO
yaani makala yote WATAALAM NISHATI, REA, TANESCO WAKAGUA MIRADI YA REA MOROGORO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATAALAM NISHATI, REA, TANESCO WAKAGUA MIRADI YA REA MOROGORO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/wataalam-nishati-rea-tanesco-wakagua.html
0 Response to "WATAALAM NISHATI, REA, TANESCO WAKAGUA MIRADI YA REA MOROGORO"
Post a Comment