title : WAZIRI JAFO ALIVALIA NJUGA SUALA LA WATU WENYE ULEMAVU WAWEZE KUPATA FURSA ZA AJIRA PAMOJA NA KUPATIWA MATIBABU BURE
kiungo : WAZIRI JAFO ALIVALIA NJUGA SUALA LA WATU WENYE ULEMAVU WAWEZE KUPATA FURSA ZA AJIRA PAMOJA NA KUPATIWA MATIBABU BURE
WAZIRI JAFO ALIVALIA NJUGA SUALA LA WATU WENYE ULEMAVU WAWEZE KUPATA FURSA ZA AJIRA PAMOJA NA KUPATIWA MATIBABU BURE
Na Victor Masangu, Kisarawe
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemean Jafo amekemea vitendo vinavyofanywa na baadhi ya jamii kuwabagua na kuwanyanyasa makundi ya watu wenye ulemavu na badala yake wabadilike na kuwashirikisha kikamilifu katika shughuli zote za kimaendeleo sambamba na kuwapatia fursa za ajira katika sekta mbali mbali ili waweze kujikwamua kiuchumi pamoja na kuondokana na wimbi la umasikini.
Jafo ametoa kauli hiyo wakati wa sherehe za ugawaji wa vifaaa saidizi kwa watu wenye ulemavu wa aina mbali mbali wanaotoka katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na wadau wa wengine wa maendeleo.
Katika hatua nyingine Waziri Jafo alimuagiza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kuhakikisha anawakatia walemavu wote bima ya afya ili waweze kutibiwa bure ili kuondokana na usumbufu ambao wamekuwa wakiupata, na kuongeza kuwa atatoa kipaumbele cha kwanza kwa watu wenye umelamvu katika fursa za ajira zilizotangazwa na serikali.
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemean Jafo (kushoto) akimkabidhi fimbo maalumu kwa ajili ya kutembelea mmoja wa watu wenye ulemavu wa macho, kulia katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakati wa halfa ya kukabidhi vifaa saidizi vikiwemo baiskeli za miguu mitatu zipatazo 40, viti vya mwendo 15 pamoja na fimbo 100.
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemean Jafo (aliyevaa suti nyeusi) akimkabidhi fimbo maalumu kwa ajili ya kutembelea mmoja wa watu wenye ulemavu wa macho,kulia katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakati wa halfa ya kukabidhi vifaa saidizi vikiwemo baiskeli za miguu mitatu zipatazo 40,viti vya mwendo 15 pamoja na fimbo 100.
Mwenyekiti wa Shirikisho la wa wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Ummy Ndariananga akitoa taarifa kwa mgeni rasmi kuhusina na changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Happiness Seneda akizngumza na walemavu na baadhi ya wananchi ambao walifika katika hafla ya ugawaji wa vifaa hivyo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiuzungumza katika halfa ya ugawaji wa vifaa hivyo kwa watu wenye ulemavu katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.(Picha Na Victor Masangu)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAZIRI JAFO ALIVALIA NJUGA SUALA LA WATU WENYE ULEMAVU WAWEZE KUPATA FURSA ZA AJIRA PAMOJA NA KUPATIWA MATIBABU BURE
yaani makala yote WAZIRI JAFO ALIVALIA NJUGA SUALA LA WATU WENYE ULEMAVU WAWEZE KUPATA FURSA ZA AJIRA PAMOJA NA KUPATIWA MATIBABU BURE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI JAFO ALIVALIA NJUGA SUALA LA WATU WENYE ULEMAVU WAWEZE KUPATA FURSA ZA AJIRA PAMOJA NA KUPATIWA MATIBABU BURE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/waziri-jafo-alivalia-njuga-suala-la.html
0 Response to "WAZIRI JAFO ALIVALIA NJUGA SUALA LA WATU WENYE ULEMAVU WAWEZE KUPATA FURSA ZA AJIRA PAMOJA NA KUPATIWA MATIBABU BURE"
Post a Comment