title : Watanzania Jiungeni Na NHIF Kabla Ya kuugua- Makinda
kiungo : Watanzania Jiungeni Na NHIF Kabla Ya kuugua- Makinda
Watanzania Jiungeni Na NHIF Kabla Ya kuugua- Makinda
Na Grace Michael, Dodoma
WATANZANIA wametakiwa kujenga utamaduni wa kuwa na bima ya afya kabla ya kuugua ili kuepukana na usumbufu wa kutafuta au kutumia gharama kubwa za matibabu wakati wanapopatwa na magonjwa.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima (NHIF), Anne Makinda wakati akizungumza na wadau kutoka Wizara zote Jijini Dodoma.
Amesema kuwa mwananchi anapokuwa na bima ya afya anakuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wowote bila kujali kama ana fedha ama hana ikilinganishwa na mwananchi ambaye hana bima ya afya ambapo akiugua ni lazima aanze kutafuta fedha za kujitibia.
“Ni lazima ifike mahali watanzania tujenge utamaduni wa kuwa na bima ya afya kabla ya kuugua, tunashuhudia namna wananchi wanavyopata shida wakati wakiwa wamefikwa na maradhi hali inayosababisha wengine hata kulazimisha kutumia njia za mkato au udanganyifu hivyo ili kuepukana na matatizo haya ni vyema tukawa na huu utamaduni wa kukata bima ya afya mapema,”alisema Mama Makinda.
Alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli imewekeza fedha nyingi katika sekta ya afya kwa kuhakikisha dawa, vifaa tiba na mahitaji yote katika vituo vya kutolea huduma vinakuwepo ili mwananchi apate huduma kamilifu.
Kutokana na hayo, aliwataka wadau hao kushirikiana na Mfuko kwa karibu kwa kutoa maoni ama ushauri wao kwa uwazi ili kuleta mabadiliko chanya ya kihuduma kwenye Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya hasa katika kipindi hiki cha kuelekea afya bora kwa wote.
Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Anne Makinda akisalimiana na mmoja wa wananchi waliokuwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa.
Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Anne Makinda akizungumza na Wadau wa Mfuko kutoka Wizara mbalimbali jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga akieleza mikakati ya Mfuko katika kufikia malengo ya kuwahudumia wananchi wengi zaidi.
Hivyo makala Watanzania Jiungeni Na NHIF Kabla Ya kuugua- Makinda
yaani makala yote Watanzania Jiungeni Na NHIF Kabla Ya kuugua- Makinda Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Watanzania Jiungeni Na NHIF Kabla Ya kuugua- Makinda mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/watanzania-jiungeni-na-nhif-kabla-ya.html
0 Response to "Watanzania Jiungeni Na NHIF Kabla Ya kuugua- Makinda"
Post a Comment