TTCL PESA YABADILI JINA NA NEMBO

TTCL PESA YABADILI JINA NA NEMBO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TTCL PESA YABADILI JINA NA NEMBO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TTCL PESA YABADILI JINA NA NEMBO
kiungo : TTCL PESA YABADILI JINA NA NEMBO

soma pia


TTCL PESA YABADILI JINA NA NEMBO

TTCL PESA, Kampuni tanzu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Corporation, ambao ni watoaji wa huduma za fedha mtandao inapenda kuwajulisha Wateja, Wadau na Umma kwa ujumla kwamba, imefanya mabadiliko ya Jina na Nembo zinazoitambulisha Kampuni hiyo. 

TTCL PESA ilizinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan tarehe 18 Julai 2017 ikiwa na lengo kuu la kuwapa Wananchi huduma za kiwango cha juu kabisa cha ubora na unafuu wa gharama za kutuma fedha, kupokea fedha, kulipia huduma na kufanya miamala mbalimbali kwa kutumia simu zao. 

Mabadiliko haya yanakuja miezi 9 baada ya TTCL PESA kuanza huduma zake kwa Mafanikio makubwa. Hatua hii ni kuridhia ushauri wa Wateja na wadau wetu waliopendekeza kufanyika mabadiliko ya jina na Nembo ili kuongeza mvuto wa huduma, kukidhi mahitaji ya Soko na urahisi wa kuitambua huduma hii miongoni mwa huduma zinazotolewa na Taasisi nyingine. 

Huduma za fedha Mtandao ni Sekta inayokua kwa kasi duniani kote. Hapa Nchini Tanzania, miamala inafanyika katika jamii kupitia njia hii na kusaidia sana katika kuokoa muda, kurahisisha manunuzi, kutoa ajira kwa Makundi mengi ya wananchi hasa Wanawake na Vijana, kuongeza Mapato ya Nchi kupitia tozo za kodi, kuongeza usalama wa fedha na kuepusha uwezekano wa vitendo vya kihalifu kama wizi na utapeli visiweze kutokea kwa urahisi. 

Kwa kutambua umuhimu wa Jina la huduma na Nembo kuwa ni nyenzo muhimu sana katika mikakati ya Biashara na hasa biashara yenye ushindani mkubwa kama hii ya Fedha Mtandao, TTCL Corporation inaamini kuwa, Jina na Nembo mpya zitakidhi mahitaji ya Wadau na Ushindani wa soko sambamba na kusaidia harakati za kuongeza kasi ya kusambaa kwa huduma za Fedha Mtandao zinazotolewa na Shirika letu kupitia Kampuni yake tanzu ya TTCL PESA. 

Tunaileta T-Pesa kuja kuwa muhimili mkuu wa miamala ya kifedha Tanzania. Tunamlenga kila mwananchi kufaidika na huduma za tpesa ambazo zimekuwa nafuu na salama zaidi. Uzinduzi wa nembo hii ni mwanzo wa mambo mazuri na makubwa yatakayoletwa na T-Pesa. Nia yetu ni kuwa sehemu ya kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi kwa kuhakikisha tunatoa suluhisho la uhakika katika miamala ya kifedha hususani katika malipo ya huduma za umma and ukusanyaji wa malipo hayo. T-Pesa itashirikiana na taasisi zote za umma, mabenki na taasisi binafsi katika kufikia malengo haya na mwisho kutoa huduma bora nafuu na za uhakika kwa watanzania. 

Imetolewa na; 
Ofisi ya Uhusiano, 
TTCL Makao Makuu, 
Dar Es Salaam. 
3 Machi, 2018


Hivyo makala TTCL PESA YABADILI JINA NA NEMBO

yaani makala yote TTCL PESA YABADILI JINA NA NEMBO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TTCL PESA YABADILI JINA NA NEMBO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/ttcl-pesa-yabadili-jina-na-nembo.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TTCL PESA YABADILI JINA NA NEMBO"

Post a Comment