title : TAASISI YA MEN AT WORK YACHANGIA DAMU KUWASAIDIA WENYE UHITAJI
kiungo : TAASISI YA MEN AT WORK YACHANGIA DAMU KUWASAIDIA WENYE UHITAJI
TAASISI YA MEN AT WORK YACHANGIA DAMU KUWASAIDIA WENYE UHITAJI
Na Woinde Shizza,Arusha
TAASISI isiyokuwa ya kiserikali ya Wanaume ya Men At Work imeendesha mchakato wa kuchangia damu kwa lengo la kutaka itumike kuwasaidia akina kinamama wanaojifungua na kupoteza damu nyingi.Pia damu hiyo itawasaidia majuruhi wanaonusurika na ajali na kufikishwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru mkoani Arusha.
Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Maxwell Stanslaus amesema leo mkoani hapa wameamua kuchangia damu kama mchango wa wanaume kujitoa kwa ajili ya jamii na kuisaidia jamii kwani wanaume ni nguzo ya familia,jamii na taifa kwa ujumla.Stanslaus amewataka wanaume wote nchini
kuwajibika na kuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii .
"Kwa sasa tumeamua kushirikiana na kitengo cha damu salama kuchangia damu ili kupunguza changamoto ya upungufu wa damu katika benki ya damu,"amesema Stanslaus .Ameongeza taasisi hiyo ina kazi ya kuwahasisha wanaume wanawajibikaji na kushiriki katika nafasi za malezi familia na jamii ili kujenga familia imara na hatimaye taifa imara.
Kwa upande wake Mwanachama wa Men At Work Rodgers Nelson amesema kuwa anajisikia faraja kuchangia damu ili kusaidia kuokoa maisha ya kinamama wajawazito ambao hupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.Kwa upande wa Melayeki amesema kwake ni mara yake ya kwanza kutoa damu, hivyo amewatoa hofu wananchi kutokua waoga wa kuchangia damu.
Mwanachama wa Taasisi ya Wanaume ya Men at work akichangia damu
Wanachama wa Taasisi ya Wanaume ya Men at work Rodgers Nelson wakichangia damu katika viwanja vya Sheikjh Amri Abeid(picha na Woinde Shizza,Arusha )
Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanaume ya Men at work Maxwell Stanslaus akizungumza na Mkazi wa Arusha katika zoezi la uchangiaji wa damu lililoendeshwa ma taasisi yake.
Hivyo makala TAASISI YA MEN AT WORK YACHANGIA DAMU KUWASAIDIA WENYE UHITAJI
yaani makala yote TAASISI YA MEN AT WORK YACHANGIA DAMU KUWASAIDIA WENYE UHITAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAASISI YA MEN AT WORK YACHANGIA DAMU KUWASAIDIA WENYE UHITAJI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/taasisi-ya-men-at-work-yachangia-damu.html
0 Response to "TAASISI YA MEN AT WORK YACHANGIA DAMU KUWASAIDIA WENYE UHITAJI"
Post a Comment