title : OFISI YA MKEMIA MKUU YATOA TUZZO WANAFUNZI BORA KEMIA NA BAIOLOJIA.
kiungo : OFISI YA MKEMIA MKUU YATOA TUZZO WANAFUNZI BORA KEMIA NA BAIOLOJIA.
OFISI YA MKEMIA MKUU YATOA TUZZO WANAFUNZI BORA KEMIA NA BAIOLOJIA.
Mwambawahabari
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Wanafunzi 24 wa kidato cha nne na sita pamoja na walimu wamefanikiwa kupewa tuzzo na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya kufanya vizuri kitaifa katika Masomo ya kemia na Baiolojia mwaka 20I6 na 20I7.
Kwa kidato cha sita mshindi wa kwanza amepata 500,000/=, pili 400,000/=, tatu 350,000/=, huku upande wa walimu wamepewa 500,000/= kila mmoja.
Akizungumza katika hafka ya kugawa tuzzo hizo Mganga Mkuu wa Serikali Prof Muhammad Bakari Kambi, amesema kuwa Masomo ya bailojia na kemia ni muhimu katika kufanikisha maendeleo hapa nchini.
Amesema kuwa masomo hayo ni muhimu, kwani watu wanaosoma masoma hayo wapo katika soko la ajira tofauti na masomo mengine.
"Taaluma ya masoma ya kemia na bailogia imekuwa ikizalisha wataalamu wengi hapa nchini ambao wamekuwa na manufaa kwa taifa" amesema Prof Kambi.
Prof Kambi ambaye alikuwa anamwakilisha mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile amefafanua kuwa changamoto iliyokuwepo ni wanafunzi kutopenda masomo ya sayansi.
Amesema kuwa wanafunzi wengi wanasoma masoma ambayo yanazalisha wataalamu katika soko la ajira tayari wamezidi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Esther Joson, amesema kuwa utoaji wa tuzzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya kemia na bailojia ni mwendelezo, kwani walianza utaratibu huo tangu mwaka 2007.
Amesema kuwa mpaka sasa wamefanikiwa kutoa tuzzo hizo kwa wanafunzi I68 pamoja na walimu I2 ambao wamefanya vizuri.
Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko, amesema kuwa lengo la kutoa tuzzo hizo ni kuleta hamasa ya wanafunzi kupenda masomo ya sayansi.
Amesema kuwa wanafunzi wanatakiwa kupenda masomo ya sayansi jambo ambalo litasaidia katika soko la ajira pamoja na kuwa wataalam wa masuala mbalimbali.
"Tunatoa tuzzo hizi ili kuwapongeza na kuleta hamasa katika kuyapenda masoma ya sayansi " amesema Mafumiko.
Mwanafunzi wa sekondari ya Kibaha ambaye ameshika nafasi ya pili kitaifa kwa somo la Kemia huku bailojia akiwa nafasi ya tatu, Paschal Joseph, ameeleza kuwa kupenda masoma hayo na kosoma kwa bidii ni miongoni mwa vitu vilivyosaidia kufanya vizuri.
Joseph ambaye amefanya vizuri masomo haya kwa kidato cha nne mwaka 20I6, amesema kuwa ili uweze kufanya vizuri zaidi jitiada binafsi zinaitajika.
Wanafunzi walipewa tuzzo na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kidato cha sita ni pamoja na Agatha Ninga-Tabora Girls, Sophia Juma-St. Mary'S, Doreen Smart- Waja Girls.
Wavulana ni Nathanael Ndagiwe-Mzumbe, Shabani Kaniki- Majengo, Benedict Msangi- Mzumbe.
Kwa kidato cha nne ni Samaiya Mussa-Zanzibar Fedha, Amira Moh'danad- Fidel Catro, Nelda John- Marian Girls, Abuubakar Ali Hassan- Fidel Castrol, Pascal Joseph-Kibaha, Benjamini Herman- Pugu.
Wengine ni Nelda John- Marian Girls, Irene Ambrose Gerald- Kifungilo Girls pamoja na Christa Kobulungo Eduward kutoka St. Francis Girls.
Walimu bora katika somo la Mkemia ni Salim Mohamed Salm kutoka shule ya Sekondari Fidel Castro pamoja na Rutigadius Benedicto wa Tabora boys.
Katika bailojia ni Mwalimu Rogasian Fissoo kutoka shule ya UWAKA Mbeya pamoja na Ibrahim Mrema wa Tabora Girls.
Hivyo makala OFISI YA MKEMIA MKUU YATOA TUZZO WANAFUNZI BORA KEMIA NA BAIOLOJIA.
yaani makala yote OFISI YA MKEMIA MKUU YATOA TUZZO WANAFUNZI BORA KEMIA NA BAIOLOJIA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala OFISI YA MKEMIA MKUU YATOA TUZZO WANAFUNZI BORA KEMIA NA BAIOLOJIA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/ofisi-ya-mkemia-mkuu-yatoa-tuzzo.html
0 Response to "OFISI YA MKEMIA MKUU YATOA TUZZO WANAFUNZI BORA KEMIA NA BAIOLOJIA."
Post a Comment