title : SERIKALI YAHIMIZA HALMASHAURI KUBUNI MIRADI YA KIMKAKATI ILI KUJIONGEZEA MAPATO
kiungo : SERIKALI YAHIMIZA HALMASHAURI KUBUNI MIRADI YA KIMKAKATI ILI KUJIONGEZEA MAPATO
SERIKALI YAHIMIZA HALMASHAURI KUBUNI MIRADI YA KIMKAKATI ILI KUJIONGEZEA MAPATO

Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Suzana Mgonukulima, aliyependekeza itungwe sheria ya kuibana serikali ikiwa haitarejesha fedha zilizotokana na vyanzo vya mapato vilivyopo kwenye Miji, Halmashauri, Manispaa na Majiji zitakazokusanywa na kuwekwa kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali.
Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 44 cha Sheria ya Bajeti, mgao wa fedha kutoka katika Mfuko Mkuu wa Serikali utazingatia bajeti iliyoidhinishwa, upatikanaji na mtiririko wa fedha, utekelezaji mpango wa ununuzi na mpango wa kuajiri hivyo hakuna Fungu litakaloruhusiwa kufanya matumizi ya aina yoyote mpaka kuwe na fedha za kulipa matumizi husika.
“Usimamizi wa Mapato hayo kwa mujibu ya Sheria ya Bajeti ya Mwaka 2015 Kifungu namba 58 unazingatia mapato kuingizwa kwenye Sheria ya Kuidhinisha Matumizi ya Fedha za Serikali, aliyepewa mamlaka ya kukusanya mapato ya Serikali atawajibika katika ukusanyaji wenye ufanisi, utunzaji wa hesabu, utoaji wa taarifa na kuzuia ufujaji wa mapato”, alisema Dkt. Kijaji.
Hivyo makala SERIKALI YAHIMIZA HALMASHAURI KUBUNI MIRADI YA KIMKAKATI ILI KUJIONGEZEA MAPATO
yaani makala yote SERIKALI YAHIMIZA HALMASHAURI KUBUNI MIRADI YA KIMKAKATI ILI KUJIONGEZEA MAPATO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAHIMIZA HALMASHAURI KUBUNI MIRADI YA KIMKAKATI ILI KUJIONGEZEA MAPATO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/serikali-yahimiza-halmashauri-kubuni.html
0 Response to "SERIKALI YAHIMIZA HALMASHAURI KUBUNI MIRADI YA KIMKAKATI ILI KUJIONGEZEA MAPATO"
Post a Comment