title : MOI SASA KUFANYA UPASUAJI KWA WAGONJWA 1000 KWA MWEZI-MAKAMU WA RAIS
kiungo : MOI SASA KUFANYA UPASUAJI KWA WAGONJWA 1000 KWA MWEZI-MAKAMU WA RAIS
MOI SASA KUFANYA UPASUAJI KWA WAGONJWA 1000 KWA MWEZI-MAKAMU WA RAIS
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
TAASISI ya Mifupa nchini MOI sasa itafanya upasuaji wa mifupa kwa wagonjwa wapatao 1000 kwa mwezi kutoka wagonjwa 500 mpaka 700 baada ya kupokea msaada wa chumba cha upasuaji na vifaa vyake kutoka kwa Serikali ya Kuwait .
Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa kuzindua na kupokea msaada wa chumba cha upasuaji na vifaa vyake vyenye thamani ya shilinigi milioni 186 leo katika Taasisi ya mifupa MOI leo jijini Dar es salaam.
“Hii ni faraja kubwa sana kwa Serikali kwani uboreshwaji wa huduma katika hospitali zetu za kibingwa kubwa kama MOI itaweza kuhudumia wagonjwa wengi Zaidi kutoka wagonjwa 700 kwa mwezi mpaka kufikia 1000 kwa mwezi” alisema Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Aidha Makamu wa Rais Samia Suluhu amesema kuwa anaishukuru Serikali ya Kuwait kupitia Balozi wake Jasem Al Najem kwa msaada huo kwani utaisaidia kwa kiasi kikubwa MOI katika kuboresha utoaji huduma hasa katika fani ya upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi hapa nchini.
Hivyo makala MOI SASA KUFANYA UPASUAJI KWA WAGONJWA 1000 KWA MWEZI-MAKAMU WA RAIS
yaani makala yote MOI SASA KUFANYA UPASUAJI KWA WAGONJWA 1000 KWA MWEZI-MAKAMU WA RAIS Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MOI SASA KUFANYA UPASUAJI KWA WAGONJWA 1000 KWA MWEZI-MAKAMU WA RAIS mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/moi-sasa-kufanya-upasuaji-kwa-wagonjwa.html
0 Response to "MOI SASA KUFANYA UPASUAJI KWA WAGONJWA 1000 KWA MWEZI-MAKAMU WA RAIS"
Post a Comment