title : Biteko Atatua Mgogoro Sugu Madini
kiungo : Biteko Atatua Mgogoro Sugu Madini
Biteko Atatua Mgogoro Sugu Madini
Ni baada ya kruhusu wananchi kijiji cha Mhandu kuendelea na uchimbaji dhahabu
Na Greyson Mwase, Shinyanga
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameruhusu wananchi wa kijiji cha Mhandu kilichopo katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga kuendelea na uchimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo la utafiti wa madini hayo lililokuwa linamilikiwa na Menan Sanga kwa kushirikiana na kampuni ya Lion Town.
Biteko aliyasema hayo leo tarehe 24 Novemba, 2018 katika mkutano wa hadhara ulioshirikisha wananchi wa kijiji cha Mhandu kilichopo katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mkoa huo yenye lengo la kusikiliza na kutatua changamoto za wachimbaji wa madini.
Katika ziara hiyo, Biteko aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha, Mbunge wa Jimbo la Msalala, Ezekiel Maige, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Simon Berege, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Shinyanga, Wataalam kutoka Wizara ya Madini pamoja na waandishi wa habari.
Biteko alisema kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Madini haiwezi kuruhusu mwekezaji kumiliki eneo pasipo kuliendeleza, kutokulipa kodi inayohitajika Serikalini huku wananchi wenye nia ya kuchimba katika eneo husika wakiendelea kuteseka.
Alisema kuwa, Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli imeweka mikakati mbalimbali ya uboreshaji wa Sekta ya Madini ikiwa ni pamoja marekebisho ya Sheria ya Madini inayotambua madini kama rasilimali za watanzania wote.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mhandu kilichopo katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga tarehe 24 Novemba, 2018 ikiwa ni sehemu ya ziara yake kwenye mkoa huo yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Mhandu kilichopo katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga akiwasilisha kero yake kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani ) kwenye mkutano wa hadhara.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia mbele) akiendelea na ziara katika eneo la uchimbaji wa chini ya ardhi kwenye Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu uliopo katika eneo la Kakola Wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) akipata maelezo jinsi shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu zinavyofanyika chini ya ardhi katika eneo la Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na msafara wake pamoja na watendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu kabla ya kushuka chini ya ardhi ili kujionea uchimbaji wa madini unavyofanyika.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati mbele) akiendelea na ziara katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu uliopo katika eneo la Kakola Wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Hivyo makala Biteko Atatua Mgogoro Sugu Madini
yaani makala yote Biteko Atatua Mgogoro Sugu Madini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Biteko Atatua Mgogoro Sugu Madini mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/biteko-atatua-mgogoro-sugu-madini.html
0 Response to "Biteko Atatua Mgogoro Sugu Madini"
Post a Comment