title : MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AZINDUA KAMATI YA MAAFA YA MKOA
kiungo : MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AZINDUA KAMATI YA MAAFA YA MKOA
MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AZINDUA KAMATI YA MAAFA YA MKOA





Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .
serikali mkoani Kilimanjaro imezindua kamati ya Maafa ya mkoa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Sheria namba 7 ya mwaka 2015 kwa lengo la kumshauri Mkuu wa mkoa kuhusu masuala ya usimamizi wa maafa na kuratibu shughuli za dharura miongoni mwa taasisi za kisekta za serikali za mitaa.
Mbali na majukumu hayo kamati hiyo pia itakuwa na wajibu wa kutafuta rasilimali kwa ajili ya usimamizi wa maafa katika mkoa,kufungamanisha mfumo wa tahadhari ya awali katika mkoa na kuwezesha uanzishaji wa mfumo wa takwimu na taarifa za maafa za mkoa kwa kushirikiana na wakala.
Akizindua kamati hiyo inayoundwa na wajumbe kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo za kidini,wafanyabiashara ,Wataalamu mbalimbali pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalma ya mkoa ,Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira alisema kwa kipindi kirefu mkoa haujawa na kamati ya maafa iliyo hai ,inayojitambua na kuwajibika ipasavyo.
“Sheria hii inatafsriri maafa kwamba ni ya kimkoa kama zaidi ya wilaya moja ndani ya mkoa imeathirika au kama wilaya,mji au manispaa husika haina uwezo wa kushughulikia tatizo hilo au kama tatizo hilolimehusisha wilaya zinazopakana ndani ya mkoa “alisema Mghwira.
Mghwira alitoa maelekzo kwa wakuu wa wilaya kuhakikisha kamati za maafa za wilaya ,kata na vijiji zinaundwa na kusimamiwa ili zitekeleze majukumu yake ipasavyo kwa mujibu wa sheria hiyo huku akiwaagiza wakulurugenzi kuwawezesha wakuu wa wilaya kuandaa utaratibu wa kutoa maelekezo kwa kamati a wilaya ,kata na vijiji .
“Hakuna haja ya kusubiri maafa yatokee ndiyo tufanye maandalizi ,tuanze sasa,kwa taarifa nilizonazo mvua bado zinaendelea ,twendeni katika maeneo yanayotuzunguka kutoa tahadhari za awali kwa wananchi wote wanaooonekana kupata madhara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha”alisema Mghwira.
Mwisho.
Hivyo makala MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AZINDUA KAMATI YA MAAFA YA MKOA
yaani makala yote MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AZINDUA KAMATI YA MAAFA YA MKOA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AZINDUA KAMATI YA MAAFA YA MKOA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/mkuu-wa-mkoa-wa-kilimanjaro-azindua_19.html
0 Response to "MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AZINDUA KAMATI YA MAAFA YA MKOA"
Post a Comment