MALEZI BORA NI MSINGI KATIKA UJENZI WA FAMILA IMARA NA TAIFA IMARA

MALEZI BORA NI MSINGI KATIKA UJENZI WA FAMILA IMARA NA TAIFA IMARA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MALEZI BORA NI MSINGI KATIKA UJENZI WA FAMILA IMARA NA TAIFA IMARA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MALEZI BORA NI MSINGI KATIKA UJENZI WA FAMILA IMARA NA TAIFA IMARA
kiungo : MALEZI BORA NI MSINGI KATIKA UJENZI WA FAMILA IMARA NA TAIFA IMARA

soma pia


MALEZI BORA NI MSINGI KATIKA UJENZI WA FAMILA IMARA NA TAIFA IMARA

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe.Sezaria Makota akiwasisitiza wazazi kuchangia ujenzi wa famila na taifa kwa kuwapa malezi bora watoto wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani iliyofanyika Wilayani Kondoa katika Mkoa wa Dodoma.

Na Mwandishi Wetu Kondoa, Dodoma

Malezi bora katika familia imesemeka ni ndio msingi wa malezi kwa watoto katika jamii yetu hivyo wazazi wanapaswa kuzingatia kutoa malezi bora kwa watoto ndani ya familia na jamii kwa ujumla ili kuwa na taifa lenye uchu wa kujiletea maendeleo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe.Vaileth Makota  wakati akisoma Hotuba ya Wziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika  maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani yaliyofanyika Wilayani Kondoa katika Mkoa wa Dodoma.

Mhe. Sezaria Makota amesema kuwa wazazi wanawajibu wa kuwalea watoto katika malezi bora na katika maadili mazuri ili kujenga taifa bora lenye watoto wanaojitambua, wanaojithamini, na wenye maadili mema ili kulitumikia Taifa.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mtoto Bibi Magreth Mussai akizungumzia umuhimu wa malezi bora katika familia na wajibu wa wazazi katika kutoa malezi hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani iliyofanyika Wilayani Kondoa katika Mkoa wa Dodoma.

Ameongeza kuwa wazazi wanatakiwa kuwa walimu kwa matendo yao kwa watoto kwani watoto wanaiga yale ambayo wazazi wanafanya hivyo tabia na mienendo yao ni kati ya vitu ambavyo vitasababisha malezi mabaya au bora kwa watoto na jamii kwa ujumla.

Amesisitiza kuwa wazazi wana wajibu wa kuwalea watoto katika malezi bora ili kujenga utu, uzalendo na upendo kwa watoto na jamii kwani malezi katika familia ni msingi katika ujenzi wa taifa linalozingatia uzalendo, maadili mema, utu na uwajibikaji katika maendeleo yao na taifa.

“Tuzingatie katika kutoa malezi bora kwa watoto wetu ili tujenge taifa bora lenye maadili mema kwa maendeleo ya taifa” alisisitiza Mhe. Sezaria

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe.Sezaria Makota akipokea bango la wadau kutoka nchi ya wanaounga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania kupinga ndoa za utotoni wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani iliyofanyika Wilayani Kondoa katika Mkoa wa Dodoma.

Kwa  upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mtoto Bibi. Magreth Mussai amesisitiza watoto na vijana kuwa na maadili kwa wazazi na wanajamii ili kujenga taifa lenye maadili na upendo.

Siku ya Familia Duniani inaadhimishwa kila Mei 15, 2018 na kwa mwaka huu inaadhimishwa ikienda na kaulimbiu isemayo “Malezi Jumuishi: Msingi wa Uzalendo, Utu na Maadili ya Familia na Taifa’’.
Nesi akimchoma mtoto wa Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Vanessa Makota Chanjo ya Saratani ya Shingo ya Kizazi katika uzinduzi wa chanjo hiyo Wilayani Kondoa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani iliyofanyika Wilayani Kondoa katika Mkoa wa Dodoma.
Wananchi wa Wilaya ya Kondoa mkoa Dodoma wakifuzatilia mambo mbalimbali katika Siku ya Familia Duniani yaliyokuwa yakifanyika katika Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma.


Hivyo makala MALEZI BORA NI MSINGI KATIKA UJENZI WA FAMILA IMARA NA TAIFA IMARA

yaani makala yote MALEZI BORA NI MSINGI KATIKA UJENZI WA FAMILA IMARA NA TAIFA IMARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MALEZI BORA NI MSINGI KATIKA UJENZI WA FAMILA IMARA NA TAIFA IMARA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/malezi-bora-ni-msingi-katika-ujenzi-wa_16.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MALEZI BORA NI MSINGI KATIKA UJENZI WA FAMILA IMARA NA TAIFA IMARA"

Post a Comment