title : Watanzania wahimizwa kuchangamkia shindano la ujasiariamali la TBL
kiungo : Watanzania wahimizwa kuchangamkia shindano la ujasiariamali la TBL
Watanzania wahimizwa kuchangamkia shindano la ujasiariamali la TBL
-Mshindi kujinyakulia kitita cha Dola 50,000/-
Kampuni ya TBL Group, chini ya kampuni yake mama ya, ABIn Bev, Imewataka watanzania kuchangamkia kushiriki shindano lililozinduliwa karibuni la wazo la ubunifu kupitia ujasiriamali, ,(The Africa Sustainability Challenge) linalolenga kukabiliana na changamoto zinazolikabili bara la Afrika na changamoto endelevu za kidunia.Ushiriki wa shindano ni kupitia tovuti ya https://ift.tt/2KvgdJj
Washiriki wa shindano ambao wazo la ubunifu la ABinBev, litaibuka na ushindi watajishindia fedha za kuwawezesha kutekeleza wazo lao kwa vitendo kiasi cha Dola za Kimarekani 50,000 (zaidi ya shilingi milioni za Tanzania.
Akiongea juu ya shindano hili jijini Dar es Salaam,Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL Group,Irene Mutiganzi,alisema “Tukiwa kampuni kubwa ambayo ina mtandao wa kidunia tuna mtazamo wa kufanya uzalishaji wa vinywaji vya bia sambamba na kupitia vinywaji hivi kuwaunganisha watu pamoja kwa miaka zaidi ya 100 ijayo,na lengo hili hili lifanikiwe tunahitaji mawazo shirikishi kutoka wadau mbalimbali nchini na barani Afrika kwa ujumla”.
Mutiganzi,alisema mawazo hayo ya ubunifu yanatakiwa kujikita jinsi ya kutatua matatizo yanayolikabili bara la Afrika ambayo baadhi yake ni kuhusu kilimo bora,changamoto ya maji,hali ya hewa na kukuza ujasiriamali endelevu.
Shindano hili la mawazo ya kukabili changamoto la AB InBev Africa linawataka washiriki kutoka nchi mbalimbali kubuni jinsi ya kukabili changamoto zinazowakabili katika maeneo yao kama vile kukuza sekta ya kilimo,upatikanaji wa maji safi ,kuimarisha mifumo ya maji taka,kuwezesha familia zenye vipato vya chini,mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuongeza wigo wa ajira kwa watu wengi katika jamii.
“Hii ni fursa pekee kwa wajasiriamali wenye mawazo ya ubunifu wa kukabiliana na changamoto zilizobainishwa kuweza kujishindia safari ya kwenda Silicone Savannah jijini Nairobi nchini Kenya sambamba na kujishindi dola za Marekani
50,000 za mtaji wa kuendeleza wazo lililoshinda pia washiriki watapata fursa ya kushiriki katika mafunzo ya kuwajengea uwezo na kushiriki katika mashindano ya ngazi ya dunia yatakayofanyika mjini Newyork nchini Marekani chini ya uratibu wa kampuni ya ABIn Bev”,alisisitiza.
Shindano hili liko wazi kwa washiriki kutoka nchi za Botswana, Ghana, Lesotho, Mozambique, Namibia, Nigeria, South Africa, Swaziland, Tanzania, Uganda na Zambia na mwisho wa kutuma ni mwisho wa mwezi huu .
Hivyo makala Watanzania wahimizwa kuchangamkia shindano la ujasiariamali la TBL
yaani makala yote Watanzania wahimizwa kuchangamkia shindano la ujasiariamali la TBL Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Watanzania wahimizwa kuchangamkia shindano la ujasiariamali la TBL mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/watanzania-wahimizwa-kuchangamkia.html
0 Response to "Watanzania wahimizwa kuchangamkia shindano la ujasiariamali la TBL"
Post a Comment