title : Ilala watakiwa kuanzisha klabu za mazingira
kiungo : Ilala watakiwa kuanzisha klabu za mazingira
Ilala watakiwa kuanzisha klabu za mazingira
MANISPAA ya Ilala jijini Dar es Salaam imeshauriwa kuanzisha klabu za mazingira katika shule zake za msingi za manispaa hiyo ili wanafunzi wafundishwe umuhimu wa utunzaji mazingira.
Ushauri huo umetolewa Dar es Salaam jana na Ofisa Tawala wa Wilaya ya Ilala Jabiri Makame wakati wa kampeni ya upandaji miti shule msingi Yongwe iliyopo Chanika Ilala.
"Naomba Idara ya Mazingira manispaa ya Ilala muunde vilabu vya mazingira katika shule zenu za msingi ili wanafunzi wafundishwe umuhimu wa utunzaji wa mazingira"amesema Makame. Makame amesema suala la utunzaji wa mazingira ni letu sote hivyo inatakiwa tuweke mikakati mbalimbali jinsi ya uendelezaji na utunzaji wa mazingara.
Afafanua ikiwekwa mikakati endelevu ya kuanzisha vilabu mashuleni wanafunzi wakafahamu jinsi utunzaji mazingira serikali itakuwa imefaidika jamii nzima itapata elimu hiyo. Amewapongeza Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa juhudi zao kwa kuwekeza shule za msingi hasa upande wa mazingira na kuwataka wadau wengine Kushirikia na serikali.
Amesema utunzaji wa mazingira unafaida nyingi nchi yetu ikiwemo ya kuepuka jangwa,faida nyingine miti huleta kivuli na miti mingine ya matunda. Kwa upande wake Ofisa Elimu Msingi Ilala Elzabeth Thomas amesema Standard Chartered wameanza kampeni ya kusaidia shule za Msingi Ilala toka mwaka 2014 mpaka sasa wameweza kupanda miti 3300.
Amesema kuanzia mwaka 2014 hadi sasa wamekuwa wakishirikiana katika utunzaji wa mazingira katika shule mbalimbali. Amesema awali kabla kupanda miti shule ya Yongwe kampeni hiyo ilianzia shule ya msingi Majani ya Chai, Pugu Kajiungeni, Buyuni, Kigogo Freshi, Viwege na Uhuru Mchanganyiko.
Kwa upande wake Ofisa wa Benki hiyo Isema Bilali amesema benki hiyo ilianza shughuli zake nchini mwaka 1917 na kwamba upandaji miti una faida nyingi ikiwemo kutuwezesha kupata mvua,ujenzi,inatupa chakula inazuia mmomonyoko wa udongo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Yongwe Kata ya Chanika wakiwa katika wiki ya mazingira na upandaji miti shuleni kwao Dar es Salaam jana Picha na Heri Shaaban
Hivyo makala Ilala watakiwa kuanzisha klabu za mazingira
yaani makala yote Ilala watakiwa kuanzisha klabu za mazingira Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Ilala watakiwa kuanzisha klabu za mazingira mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/ilala-watakiwa-kuanzisha-klabu-za.html
0 Response to "Ilala watakiwa kuanzisha klabu za mazingira"
Post a Comment