title : ESRF, Ubalozi wa Sweden na UDSM waandaa Mdahalo wa Uchumi Jumuishi
kiungo : ESRF, Ubalozi wa Sweden na UDSM waandaa Mdahalo wa Uchumi Jumuishi
ESRF, Ubalozi wa Sweden na UDSM waandaa Mdahalo wa Uchumi Jumuishi
TANZANIA itahitaji kutengeneza mkakati mpya wa maendeleo na kuachana na falsafa za zamani kama itataka kufikia ustawi na kuwa nchi yenye kipato cha Kati.
Mkakati huo katika; masoko, rasilimali na uwezeshaji unatakiwa kuwezesha sera za maendeleo zilizo endelevu kwa kuangalia zaidi changamoto tofauti za maendeleo na kuzikabili kabla ya kuzitumia kubadili harakati za maendeleo.
Kauli hiyo imo katika mdahalo uliofanyika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na kuongozwa wataalamu wa uchumi.
Walisema katika mdahalo huo kwamba mkakati wa zamani kuhusu maendeleo kwa kutegemea kuzalisha bidhaa na kuziuza nje una vikwazo vingi hasa katika uzalishaji kutokana na masuala ya teknolojia na hivyo mkakati utakaokuwa jumuishi, unaoratibu kilimo, madini na huduma unaweza kuwezesha kukua kwa uchumi kama ilivyokuwa katika mkakati wa zamani wa uzalishaji kwa ajili ya kupeleka nje.
Wamesema katika mkakati huo mpya serikali inatakiwa kufanya wajibu mkubwa kufanya mabadiliko ya kimfumo na kimkakati kuelekea uchumi jumuishi ambapo kila mwananchi atashiriki.
Uchumi huo hautategemea uzalishaji wa viwandani pekee bali uchumi wa kisasa unaozingatia huduma ambao katika awamu ijayo kilimo cha kisasa nchini Tanzania kitakuwa sehemu ya mkakati huo.
Wanazuoni hao wamesema kwamba mafanikio ya kuwa na uchumi jumuishi kwa nadharia za sasa zinategemea mpango mkakati wa maendeleo wenye kuangalia mambo mengi yatakayowezesha kuwa na ukuaji jumuishi, unaoshirikisha na kuzingatia uwiano wa masoko, serikali na jamii.
Walisema taratibu hizo mpya duniani zitasaidia kuwa na uchumi wenye mafanikio unaobadili maisha ya watu kwa kuangalia changamoto mbalimbali ikiwamo vifo na kutengeneza mfumo mpya wenye kuzingatia uwezo na mahitaji.
Profesa wa Uchumi wa Chuo Kikuu Cornel, Ithaca na aliyekuwa mchumi wa Benki ya Dunia Prof. Kaushik Basu akiwasilisha mada kuhusu misingi ya maendeleo kwa kuzingatia sosholojia na saikolojia ya watu wakati wa mdahalo kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Aliyekuwa mchumi wa zamani wa Benki ya Dunia kutoka Chuo Kikuu cha Columbia, Prof. Joseph Stiglitz akiwasilisha mada kuhusu kutoka uzalishaji unaolenga soko la nje hadi ukuaji uchumi jumuishi wa karne ya 21 kwa taifa la Tanzania wakati wa mdahalo uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Mwenyekiti wa mdahalo kutoka kigoda cha Mwl. Julius Nyerere, Prof. Benno Ndulu akiongoza mdahalo kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jehovaness Aikaeli akitoa neno la shukrani kwa washiriki wa mdahalo kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akizungumza na kituo cha Habari cha ITV kuhusu mdahalo huo na manufaa yake kwa Tanzania na kwa sekta ya uchumi wakati wa mdahalo kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wakitoa maoni ya mdahalo kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mdahalo kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Meza kuu katika picha ya pamoja na wadau mara baada ya kumalizika kwa mdahalo kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa UDSM mara baada ya kumalizika kwa mdahalo kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala ESRF, Ubalozi wa Sweden na UDSM waandaa Mdahalo wa Uchumi Jumuishi
yaani makala yote ESRF, Ubalozi wa Sweden na UDSM waandaa Mdahalo wa Uchumi Jumuishi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ESRF, Ubalozi wa Sweden na UDSM waandaa Mdahalo wa Uchumi Jumuishi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/esrf-ubalozi-wa-sweden-na-udsm-waandaa.html
0 Response to "ESRF, Ubalozi wa Sweden na UDSM waandaa Mdahalo wa Uchumi Jumuishi"
Post a Comment