title : DKT. ASHATU KIJAJI AZIPONGEZA BENKI KUSHUSHA RIBA ZA MIKOPO
kiungo : DKT. ASHATU KIJAJI AZIPONGEZA BENKI KUSHUSHA RIBA ZA MIKOPO
DKT. ASHATU KIJAJI AZIPONGEZA BENKI KUSHUSHA RIBA ZA MIKOPO
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Uamuzi wa Serikali wa kupunguza kiwango cha chini cha amana kinachotakiwa kuwekwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na benki za biashara nchini, umechochea taasisi za fedha yakiwemo mabenki kuanza kupunguza viwango vya riba ya mikopo hatua itakayochochea ukuaji wa uchumi.
Hayo yalisemwa Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji wakati wa kufunga warsha ya wadau wa Sekta ya Fedha uliowashirikisha wabunge, washirika wa Maendeleo, wakuu wa Taasisi za fedha na Wizara ya Fedha na Mipango.
Dkt. Kijaji, alisema kuwa Serikali kupitia Benki Kuu imeshusha riba ya mikopo kwa taasisi za fedha kutoka asilimia 16.0 hadi asilimia 9.0 na kupunguza kiwango cha chini cha amana kinachotakiwa kuwekwa katika Benki hiyo na benki za biashara kutoka asilimia 10.0 hadi asilimia 8.0 kuanzia mwezi Aprili 2017, jambo ambalo limeleta matokeo chanya katika kuimarisha uwezo wa taasisi kukopesha wateja wao.
Miongoni mwa Benki zilizoshusha viwango vyao vya riba za mikopo ni CRDB ambayo imetangaza kushusha riba kutoka asilimia 22 hadi 16 na kuongeza kiasi cha kukopa kwa wafanyakazi kutoka Sh. milioni 50 hadi Sh. milioni 100 huku muda wa kurejesha ukiongezwa kutoka miaka mitano hadi saba.
Benki nyingine ni NMB ambayo imeongeza muda wa marejesho ya mikopo kwa wafanyakazi, wajasiriamali wadogo na wakubwa kutoka miezi 60 hadi 72, na imepunguza riba ya mikopo kwa wafanyakazi kutoka asilimia 21 hadi 19 na wajasiriamali wadogo kutoka asilimia 23 hadi 21.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akifunga warsha ya wadau wa Sekta ya Fedha iliyolenga kujadili mchango wa sekta hiyo katika kukuza uchumi wa viwanda leo Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu akizungumza wakati wa kufunga warsha ya wadau wa Sekta ya Fedha iliyolenga kujadili mchango wa sekta hiyo katika kukuza uchumi wa viwanda leo Jijini Dodoma.
Mbunge wa Jango’mbe Mhe. Ally Hassan King akizungumza wakati wa kufunga warsha ya wadau wa Sekta ya Fedha iliyolenga kujadili mchango wa sekta hiyo katika kukuza uchumi wa viwanda leo Jijini Dodoma.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Dkt. Honest Ngowi akiongoza mjadala wakati wa warsha ya wadau wa sekta ya fedha iliyolenga kujadili mchango wa sekta hiyo katika kukuza uchumi wa viwanda leo Jijini Dodoma.
Mmoja wa wadau wa Sekta ya Fedha akizungumzia umuhimu wa ushirikishwaji wa sekta hiyo katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo hapa nchini ili kuchochea maendeleo.
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA), Dkt. Boghayo Saqware akizungumzia hoja mbalimbali zilizoibuliwa na wajumbe wa warsha ya wadau wa sekta ya fedha iliyolenga kujadili mchango wa sekta hiyo katika kukuza uchumi wa viwanda leo Jijini Dodoma.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala DKT. ASHATU KIJAJI AZIPONGEZA BENKI KUSHUSHA RIBA ZA MIKOPO
yaani makala yote DKT. ASHATU KIJAJI AZIPONGEZA BENKI KUSHUSHA RIBA ZA MIKOPO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DKT. ASHATU KIJAJI AZIPONGEZA BENKI KUSHUSHA RIBA ZA MIKOPO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/dkt-ashatu-kijaji-azipongeza-benki.html
0 Response to "DKT. ASHATU KIJAJI AZIPONGEZA BENKI KUSHUSHA RIBA ZA MIKOPO"
Post a Comment