title : AGAPE YAENDESHA KONGAMANO KWA WANAFUNZI SHULE 8 ZA KATA YA USANDA SHINYANGA
kiungo : AGAPE YAENDESHA KONGAMANO KWA WANAFUNZI SHULE 8 ZA KATA YA USANDA SHINYANGA
AGAPE YAENDESHA KONGAMANO KWA WANAFUNZI SHULE 8 ZA KATA YA USANDA SHINYANGA
Shirika la Agape AIDS Control Programme (AACP) limeendesha kongamano kwa wanafunzi 120 kutoka shule nane zilizopo katika kata Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (Vijijini) kwa lengo la kuwajengea uelewa wanafunzi kuhusu masuala ya afya ya uzazi na ujinsia.
Kongamano hilo lililoongozwa na mdahalo wenye mada "Je Kijana akibalehe/akivunja ungo anakuwa tayari kuoa/kuolewa au kufanya ngono?" limefanyika leo Jumapili Mei 13,2018 katika ukumbi wa Ibanza Hotel uliopo mjini Shinyanga.
Mbali na kuongozwa na mada hiyo,pia wanafunzi hao wameonesha michezo kadha wa kadha huku mada mbalimbali zikitolewa ikiwemo huduma rafiki kwa vijana,ukatili wa kijinsia na madhara yake,majukumu ya afisa ustawi wa jamii na mazingira rafiki shuleni pamoja na umuhimu wa michezo.
Awali akizungumza, Afisa Mradi wa Elimu ya Afya ya Uzazi na Ujinsia kwa Vijana unaotekelezwa na shirika la AGAPE kwa ufadhili wa shirika la Kimataifa la Sida kutoka SWEDEN , Lucy Maganga alizitaja shule hizo kuwa ni shule za msingi Busanda,Nzagaluba,Manyada,Shingida,Shabuluba na shule za sekondari Usanda,Singita na Samuye.“Mdahalo huu umelenga kuwajengea uelewa wanafunzi kujiepusha na tabia hatarishi zinazoweza kusababisha wapate mimba wakiwa shuleni na magonjwa ya zinaa ukiwemo Ukimwi”,alieleza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE, John Myola akifungua mdahalo akifungua mdahalo huo ambapo aliwataka wanafunzi hao kuepuka tabia hatarishi zinazoweza kusababisha wakatishe masomo yao mfano kupata mimba wakiwa shuleni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE, John Myola akizungumza ukumbini. Kushoto ni Afisa Elimu kata ya Usanda Essero Ashery, kulia ni Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Atupokile Maseta aliyehudhuria mdahalo huo kwa niaba ya Afisa Ustawi wa jamii wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wanafunzi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE, John Myola ukumbini.
Afisa Mradi wa Elimu ya Afya ya Uzazi na Ujinsia unaotekelezwa na shirika la AGAPE ,Lucy Maganga akitoa mwongozo wa kuchangia mada ya '"Je Kijana akibalehe/akivunja ungo anakuwa tayari kuoa/kuolewa au kufanya ngono?".
Hivyo makala AGAPE YAENDESHA KONGAMANO KWA WANAFUNZI SHULE 8 ZA KATA YA USANDA SHINYANGA
yaani makala yote AGAPE YAENDESHA KONGAMANO KWA WANAFUNZI SHULE 8 ZA KATA YA USANDA SHINYANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AGAPE YAENDESHA KONGAMANO KWA WANAFUNZI SHULE 8 ZA KATA YA USANDA SHINYANGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/agape-yaendesha-kongamano-kwa-wanafunzi.html
0 Response to "AGAPE YAENDESHA KONGAMANO KWA WANAFUNZI SHULE 8 ZA KATA YA USANDA SHINYANGA"
Post a Comment