title : ZAIDI YA KAYA 200 KATA YA MNYANJANI JIJINI TANGA KUNUFAIKA NA MRADI WA UJENZI WA MTARO
kiungo : ZAIDI YA KAYA 200 KATA YA MNYANJANI JIJINI TANGA KUNUFAIKA NA MRADI WA UJENZI WA MTARO
ZAIDI YA KAYA 200 KATA YA MNYANJANI JIJINI TANGA KUNUFAIKA NA MRADI WA UJENZI WA MTARO
ZAIDI ya kaya 200 katika mtaa wa Mnyanjani kata ya Myanjani Jijini Tanga zitanufaika na mradi wa ujenzi wa mtaro kwa ajili ya kuondoa tatizo la mafuriko linalotokea kila nyakati za msimu wa mvua.
Hayo yamebainishwa na Mhandisi toka Wakala wa Usimamizi wa barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoani Tanga Omari Saidi wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya jitihada za kuzinusuru kata hizo.
Mhandisi Saidi alisema mradi huo unaokadiriwa kutumia Shilingi Milioni 170 umeelekezwa katika eneo hilo lililokuwa na hali ya kutuama kwa maji kila mwaka nyakati zote za mvua na kusababisha mafuriko na kupelekea wananchi kulazimika kuyahama makazi yao. Alisema mradi wa mtaro huo ambao utakuwa na urefu wa mita 512 utakuwa na uwezo wa kusukuma maji kuelekea bahari na kuzifanya kaya hizo na maeneo ya pembezono mwa mtaa huo kuishi kwa amani hasa nyakati za mvua.
“Ni kweli hali ya mtaa huu haikua ya kuridhisha sisi tarura ambao tunamamlaka sasa tumeona hiki ndio kipindi cha kurekebisha miundombinu ya mifereji namea mvua zitakapo nyesha kaya hizi zitakuwa sehemu salama”Alisema Saidi. Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Tanga(CUF) Alhaj Mussa Mbaruku ambae alitembelea mradi huo jana alisema matumaini makubwa yanaonekana ya kuwanusuru wananchi hao na mafuriko yanayotokea kila mwaka.
Alhaj Mbaruku alisema eneo hilo limekuwa kero kwa wananchi hao ambao kila nyakati za mvua maisha yao yanakuwa hatarini kutokana na hofu ya mafuriko yanayosababishwa na mvua za misimu na kulazimika kutafuta makzi mapya.
“Taratibu hali ya maeneo yaliyokuwa yanakumbwa na mafuriko ndani ya Jiji yanaanza kuwa na hali nzuri baada ya taasisi hiyo kuwa makini na utekelezaji wa ujenzi wa mifereji hasa katika maeneo yanayotuama maji”Alisema Alhaj Mbaruku. Hata hivyo aliiomba taasisi hiyo kuendeleza kasi yao na mbali ya miradi ya mifereji pia ihakikishe kuwa barabara zote ndani ya Jiji hili zinaweza kutumika nyakati zote na zinajengwa kwa kiwango cha lami huku akiongeza kusema kuwa ulazima wa uwepo wa barabara za lami ndani ya jiji lazima uzingatiwe.
Awali akizungumzia kero hiyo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Bakari Haule alisema tatizo la mafuriko katika eneo hilo lililkua ni kubwa mbali ya nyumba hizo kujengwa katika mpangilio lakini adha kubwa ilikuwa ni kutuama kwa maji nyakati za mvua.
Hivyo makala ZAIDI YA KAYA 200 KATA YA MNYANJANI JIJINI TANGA KUNUFAIKA NA MRADI WA UJENZI WA MTARO
yaani makala yote ZAIDI YA KAYA 200 KATA YA MNYANJANI JIJINI TANGA KUNUFAIKA NA MRADI WA UJENZI WA MTARO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ZAIDI YA KAYA 200 KATA YA MNYANJANI JIJINI TANGA KUNUFAIKA NA MRADI WA UJENZI WA MTARO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/zaidi-ya-kaya-200-kata-ya-mnyanjani.html
0 Response to "ZAIDI YA KAYA 200 KATA YA MNYANJANI JIJINI TANGA KUNUFAIKA NA MRADI WA UJENZI WA MTARO"
Post a Comment