title : WAZIRI MHAGAMA AMTAKA MSAJILI WA VYAMA KUCHUKUA HATUA KWA VYAMA VINAVYOKIUKA SHERIA NA MIONGOZO ILIYOPO
kiungo : WAZIRI MHAGAMA AMTAKA MSAJILI WA VYAMA KUCHUKUA HATUA KWA VYAMA VINAVYOKIUKA SHERIA NA MIONGOZO ILIYOPO
WAZIRI MHAGAMA AMTAKA MSAJILI WA VYAMA KUCHUKUA HATUA KWA VYAMA VINAVYOKIUKA SHERIA NA MIONGOZO ILIYOPO
Waziri wa Nchi Ofisi anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amemuagiza Msajili wa vyama vya Siasa kuchukua hatua kwa vyama vinavyokiuka sheria na miongozo ya vyama vya siasa.
Ametoa kauli hiyo Aprili 23, 2018 alipokuwa akitoa maelezo ya ufafanuzi juu ya hoja za ofisi yake, zilizoainishwa katika Ripoti ya Mthibiti na Ukaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa fedha unoishia Juni 30, 2018 alipokutana na waandishi wa habari Bungeni Dodoma.
Waziri Mhagama ameelekeza kuhakikisha vyama vyenye mapungufu upande wa hesabu zao basi wawasilishe kwa Msajili wa vyama ndani ya wiki 3 hadi 4.
“Namtaka Msajili wa Vyama achukue hatua za Kisheria pasi kusita kwa chama chochote kinachokiuka sheria ya vyama vya siasa Na. 2 ya mwaka 1992”.alisema Waziri Mhagama
Aidha amemtaka Msajili wa Vyama vya siasa nchini kuhakikisha anaweka miongozo na mpango kazi ili vyama vilivyozoea kutowasilisha hesabu zao viache mara moja kwa mujibu wa sheria.
Waziri Mhagama aliongezea kuwa taarifa ya Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ilibaini mapungufu kadhaa katika uendeshaji wa vyama vya siasa ikiwemo; Upungufu katika hesabu zilizowasilishwa chini ya viwango vya Kimataifa vya uandaaji wa hesabu katika sekta za umma na baadhi ya vyama kushindwa kuwasilisha hesabu zao kwa CAG kwa ukaguzi
Pamoja na hayo alibainisha kuwepo kwa vyama vya kisiasa visivyotumia rejista ya mali za kudumu ambapo vyama vinne ikiwemo;CHADEMA, NLD,ADC na Demokrasia Makini havina Daftari la kudumu la mali zao ikiwa ni kinyume na sheria zilizopo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari juu ya Ufafanuzi wa Hoja za ofisi yake zilizoainishwa katika Ripoti ya Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa fedha unoishia Juni 30, 2018 Bungeni Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano ulioandaliwa na Idara ya Habari Maelezo, Kwa Mawaziri walipokutana kutoa ufafanuzi kwa baadhi ya hoja zilizoainishwa katika Ripoti ya Mthibiti na Ukaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa fedha unoishia Juni 30, 2018.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiteta jambo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi wakati wa mkutano na waandishi wa habari Dodoma Aprili 23, 2018.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas akizungumza na waandishi wa habari Bungeni Dodoma. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAZIRI MHAGAMA AMTAKA MSAJILI WA VYAMA KUCHUKUA HATUA KWA VYAMA VINAVYOKIUKA SHERIA NA MIONGOZO ILIYOPO
yaani makala yote WAZIRI MHAGAMA AMTAKA MSAJILI WA VYAMA KUCHUKUA HATUA KWA VYAMA VINAVYOKIUKA SHERIA NA MIONGOZO ILIYOPO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MHAGAMA AMTAKA MSAJILI WA VYAMA KUCHUKUA HATUA KWA VYAMA VINAVYOKIUKA SHERIA NA MIONGOZO ILIYOPO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/waziri-mhagama-amtaka-msajili-wa-vyama.html
0 Response to "WAZIRI MHAGAMA AMTAKA MSAJILI WA VYAMA KUCHUKUA HATUA KWA VYAMA VINAVYOKIUKA SHERIA NA MIONGOZO ILIYOPO"
Post a Comment