title : WANAFUNZI WA TANZANIA WANAOSOMA CHUO KIKUU CHA SHARDA INDIA WASHEREHEKEA SIKUKUU YA MUUNGANO
kiungo : WANAFUNZI WA TANZANIA WANAOSOMA CHUO KIKUU CHA SHARDA INDIA WASHEREHEKEA SIKUKUU YA MUUNGANO
WANAFUNZI WA TANZANIA WANAOSOMA CHUO KIKUU CHA SHARDA INDIA WASHEREHEKEA SIKUKUU YA MUUNGANO
Na Emmanuel Masaka, Globu ya jamii
WANAFUNZI wa kitanzania wasoma katika Chuo kikuu cha Sharda nchini India jana Aprili 26 wamesherekea Sikukuu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na hiyo ni katika kuadhimisha miaka 54 ya Muungano.
Sherehe hiyo imefanyika kupitia kampuni ya Global Education link inayohusika na masomo ya elimu ya juu nje ya nchi ambapo wanafunzi wa kitanzania wanaosoma katika chuo hicho kupitia kampuni ya Gobal Education link ya nchini Tanzania sambamba na viongozi na wamiliki wa Chuo hicho wamepata nafasi ya kusheherekea siku hiyo.
Akizungumza sherehe hizo Mkurugenzi wa kitengo cha Kimataifa Ashock Daryani ameiambia Michuzi Blog kuwa Taifa la Tanzania ni kubwa na lenye watu wengi na katika Chuo Kikuu cha Sharda anajivunia kuwa na mwanafunzi bora chuoni hapo na kubwa zaidi wamefurahia kushiriki kwenye kusherehekea Sikuu ya Muungano kwa wanafunzi wao wanaosoma nchini humo.
Pia amefafanua kwa baadaye Afrika itakuwa ni bara linaloongoza katika soko la uchumi duniani na hiyo ni kutokana na uwepo wa rasilimali za kutosha, na wasomi wengi wanachohitaji ni kuwa na uongozi imara na thabiti huku akielezea hatua ambazo zinachukuliwa na Serikali ya Awamu ya tano katika kuhakikisha rasilimali zinanufaisha Watanzania wote na kujenga uchumi imara.
Amewataka wanafunzi hao wa Tanzania wanasoma kwenye chuo hicho kuhakikisha baada ya kuhitimu masomo wanatumia elimu na maarifa ambayo wameyapata katika kuendeleza nchi.Kwa upande wa Anitha Boaz Ituwe ambaye ni mwanafunzi wa Shahada ya Sheria mwaka wa nne na Mwakilishi wa wanafunzi wa Tanzania chuoni Sharda ameeleza dhumuni ya kusherekea Muungano ni kujumuika na watanzania wengine katika kudumisha muungano.
Ameongeza wamefurahi wa kujumuika na wanafunzi kutoka mataifa mengine kama Uganda na Nigeria.Aidha maadhimisho yao yalienda sambamba na maonesho mbalimbali kama ngoma na maonesho ya mavazi.
Baadhi ya Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma kwenye chuo hicho wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo
Hivyo makala WANAFUNZI WA TANZANIA WANAOSOMA CHUO KIKUU CHA SHARDA INDIA WASHEREHEKEA SIKUKUU YA MUUNGANO
yaani makala yote WANAFUNZI WA TANZANIA WANAOSOMA CHUO KIKUU CHA SHARDA INDIA WASHEREHEKEA SIKUKUU YA MUUNGANO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAFUNZI WA TANZANIA WANAOSOMA CHUO KIKUU CHA SHARDA INDIA WASHEREHEKEA SIKUKUU YA MUUNGANO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/wanafunzi-wa-tanzania-wanaosoma-chuo.html
0 Response to "WANAFUNZI WA TANZANIA WANAOSOMA CHUO KIKUU CHA SHARDA INDIA WASHEREHEKEA SIKUKUU YA MUUNGANO"
Post a Comment