title : SERIKALI KUWANUFAISHA WACHIMBAJI WADOGO-MAJALIWA
kiungo : SERIKALI KUWANUFAISHA WACHIMBAJI WADOGO-MAJALIWA
SERIKALI KUWANUFAISHA WACHIMBAJI WADOGO-MAJALIWA
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali imeweka mikakati mizuri kuhakikisha wananchi hususani wachimbaji wadogo wadogo wananufaika na uwepo wa rasilimali hiyo.
Hivyo, Waziri Mkuu amewashauri wachimbaji wadogo wadogo wajiunge katika vikundi ili Serikali iweze kuwapatia misaada mbalimbali ikiwemo mkopo ili waongeze mitaji.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Novemba 29, 2018) alipozungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi jengo la halmashauri ya Mbogwe.Amewahamasisha wachimbaji hao watumie taasisi mbalimbali za kifedha na kukopa fedha na kununua mitambo ya uchimbaji na uchenjuaji kwa lengo la kujiongozea tija.
Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Geita kwa ziara ya kikazi, amesema wachimbaji wadogo wadogo waendelee kuwa na imani na Serikali yao, kwa kuwa imewapangia mambo mazuri.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewahakikishia wananchi wa wilaya hiyo kwamba Serikali imedhamilia kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.
Amesema katika kumaliza tatizo la maji Serikali imetoa zaidi ya sh. bilioni moja kwa ajili ya uchimbaji visima virefu 11 na visima vifupi 43 katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.Amesema Serikali ya Awamu ya Tano ina mikakati ya kumaliza tatizo la maji nchini kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa Hadhara kwenye Kiwanja cha Shule ya Msingi ya Masumbwe wilayani Mbogwe, Novemba 29, 2018.
Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Mkutano wa Hadhara kwenye Kiwanja cha Shule ya Msingi ya Masumbwe wilayani Mbogwe, Novemba 29, 2018.
Wananchi wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipoingia kwenye Kiwanja cha Shule ya Misngi ya Masumbwe wilayani Mbogwe kuhutubia Mkutano wa Hadhara, Novemba 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Mkutano wa Hadhara kwenye Kiwanja cha Shule ya Msingi ya Masumbwe wilayani Mbogwe, Novemba 29, 2018.
Wananchi wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipoingia kwenye Kiwanja cha Shule ya Misngi ya Masumbwe wilayani Mbogwe kuhutubia Mkutano wa Hadhara, Novemba 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Hivyo makala SERIKALI KUWANUFAISHA WACHIMBAJI WADOGO-MAJALIWA
yaani makala yote SERIKALI KUWANUFAISHA WACHIMBAJI WADOGO-MAJALIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUWANUFAISHA WACHIMBAJI WADOGO-MAJALIWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/serikali-kuwanufaisha-wachimbaji-wadogo_67.html
0 Response to "SERIKALI KUWANUFAISHA WACHIMBAJI WADOGO-MAJALIWA"
Post a Comment