title : TFDA,TBS WAINGIA MAKUBALIANO KUFANYA KAZI KWA PAMOJA KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA
kiungo : TFDA,TBS WAINGIA MAKUBALIANO KUFANYA KAZI KWA PAMOJA KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA
TFDA,TBS WAINGIA MAKUBALIANO KUFANYA KAZI KWA PAMOJA KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA),imeingia makubaliano ya miaka mitatu na Shirika la Viwango nchini (TBS) katika kufanya kazi kwa ushirikiano kuhakikisha wajasiriamali na wafanyabiashara wanahudumiwa katika kukuza kazi zao.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Agness Kejo wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa pamoja kati ya watendaji wa TFDA na TBS,ambapo amesema amesema kuwa changamoto za wafanyabishara na wajasiriamali ni vema zikapatiwa ufumbuzi wake ili watimize malego yao kwa maslahi ya Taifa.
Amefafanua kwenye ujenzi wa viwanda nchini kunategemea mashirika ya TBS na TFDA katika kuviwezesha viwanda nchini kuzalisha bidhaa bora na hatimaye kuwa na uhakika wa soko la ndani na nje ya nchi.
Amesisitiza hakuna sababu ya mjasiriamali au mfanyabishara kutumia muda mwingi kupata huduma kutoka TBS au TFDA , hivyo ni vema wakashirikiana katika kuondoa changamoto ambazo zipo na huenda zinakwaza wadau hao muhimu katika maendeleo ya nchi
Kejo ameongeza watendaji katika pande mbili hizo ni lazima waendane na azma ya Serikali ya kuwa Tanzania ya viwanda kuwasaidia afanyabiashara na wajasiriamali kupata elimu kuhusu bidhaa watazozalisha kwa kuzingatia ubora.Aidha amesema ushirikiano huo umefanyika na shirika la Viwango
Zanzibar ikiwa ni kujenga Tanzania kwa pamoja katika kufikia uchumi wa kati watanzania.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Agness Kejo akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kati watendaji wa TFDA na TBS katika vituo vya kanda na ipakani kufanya kazi kwa ushirikiano kutokana na makubaliano yaliyofikiwa na taasisi hizo, jijini Dar es Salaam.
aimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula (TFDA), Justin Makisi akizungumza kuhusiana na ufunguzi na mada zitakazojadiliwa katika kufanya kazi kama timu, jijini Dar es Salaam.
03. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Agness Kejo akiwa katika picha ya pamoja watendaji wa TFDA na TBS
Hivyo makala TFDA,TBS WAINGIA MAKUBALIANO KUFANYA KAZI KWA PAMOJA KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA
yaani makala yote TFDA,TBS WAINGIA MAKUBALIANO KUFANYA KAZI KWA PAMOJA KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TFDA,TBS WAINGIA MAKUBALIANO KUFANYA KAZI KWA PAMOJA KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/tfdatbs-waingia-makubaliano-kufanya.html
0 Response to "TFDA,TBS WAINGIA MAKUBALIANO KUFANYA KAZI KWA PAMOJA KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA"
Post a Comment