title : TCAA YAAGIZWA KUSIMAMIA USAFIRI WA ANGA
kiungo : TCAA YAAGIZWA KUSIMAMIA USAFIRI WA ANGA
TCAA YAAGIZWA KUSIMAMIA USAFIRI WA ANGA
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ameitaka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), kusimamia usafiri wa anga kwa kuzingatia taratibu na kanuni za usafiri huo ili kuweka uwiano wa haki kwa waendeshaji na abiria wanaotumia usafiri huo.
Ametoa kauli hiyo mjini Dodoma wakati akizindua rasmi Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo na kuwapongeza kwa kuamua kuweka mikakati ya kununua rada nne kwa kutumia fedha za ndani.
“Lazima msimamie kanuni na taratibu zilizopo, wajibu wenu ni kutoa haki kwa watumiaji na abiria kwa usawa, hatutaki kusikia mnakandamiza watumiaji wa usafiri na mkisimamia vizuri eneo hili mtafanya idadi ya watumiaji kuongezeka na makampuni kuendelea kuwekeza zaidi kwenye usafiri” amesisitiza Prof. Mbarawa.
Waziri Prof. Mbarawa amesema yeyote anaevunja taratibu zilizowekwa kwenye usafiri wa anga Mamlaka hiyo ichukue hatua stahiki kulingana na taratibu zilizopo ili usafiri huo uweze kuwa na nidhamu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari wakati akitoa maelezo ya awali kabla ya ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi la Mamlaka hiyo, mjini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi la Mamlaka hiyo, lililofanyika mjini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari nyaraka mbalimbali mara baada ya kulifungua mjini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) lililofanyika mjini Dodoma.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala TCAA YAAGIZWA KUSIMAMIA USAFIRI WA ANGA
yaani makala yote TCAA YAAGIZWA KUSIMAMIA USAFIRI WA ANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TCAA YAAGIZWA KUSIMAMIA USAFIRI WA ANGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/tcaa-yaagizwa-kusimamia-usafiri-wa-anga.html
0 Response to "TCAA YAAGIZWA KUSIMAMIA USAFIRI WA ANGA"
Post a Comment