title : TANAPA YAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 50 KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU MKOANI SIMIYU
kiungo : TANAPA YAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 50 KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU MKOANI SIMIYU
TANAPA YAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 50 KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU MKOANI SIMIYU
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini .
Shirika la Hifadhi za Taifa leo limekabidhi mchango wa Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa shule tatu za vipaji maalumu katika mkoa wa Simiyu za Simiyu Ufundi , Simiyu Wavulana na Simiyu Wasichana .
Mchango huo umekabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka.
Fedha hizi zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa shule maalum ya sekondari ya ufundi mkoani Simiyu ikiwa ni mojawapo ya mikakati ya mkoa katika kuimarisha sekta ya elimu ambapo pia mkoa umepanga kuje nga shule nyingine maalum mbili za sekondari za wasichana na wavulana.
Kwa pamoja Mhe Mtaka aliyeambatana na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga waliahidi kuzitumia fedha hizo kama zilivyokusudiwa na kuahidi kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha umuhimu wa wananchi kuheshimu sekta ya uhifadhi kwa kuwa ina manufaa makubwa kwao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi aliahidi kuendelea kuwaunga mkono wana Simiyu kwa kuwa mkoa huo umekuwa mstari sa mbele katika kusimamia sheria za hifadhi hususan Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kuzuia uingizaji wa mifugo pamoja na majangili.
Shule ya Ufundi ya Simiyu inatarajiwa kugharimu kiasi cha Shilingi Milioni 350 hadi itakapokamilika na wadau mbalimbali wameombwa kuunga mkono jitihada hizo za Simiyu.



Hivyo makala TANAPA YAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 50 KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU MKOANI SIMIYU
yaani makala yote TANAPA YAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 50 KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU MKOANI SIMIYU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TANAPA YAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 50 KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU MKOANI SIMIYU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/tanapa-yakabidhi-hundi-ya-shilingi.html
0 Response to "TANAPA YAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 50 KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU MKOANI SIMIYU"
Post a Comment