title : SIMBA YAIVUTIA KASI MBEYA CITY, WAENDELEA NA MAZOEZI
kiungo : SIMBA YAIVUTIA KASI MBEYA CITY, WAENDELEA NA MAZOEZI
SIMBA YAIVUTIA KASI MBEYA CITY, WAENDELEA NA MAZOEZI
Na Zainab Nyamka, Globu ya jamii
KIKOSI cha Simba kimeendelea na mazoezi yake katika Uwanja wa Boko Veterani kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Mbeya hapo kesho.
Mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Taifa utawakutanisha timu hizo huku Mbeya City akitaka kujinasua kutoka katika hatari ya kunusa kushuka daraja huku Simba wakitaka kuendelea kukalia kiti cha uongozi wa ligi.
Kikosi hicho cha Simba kinajifua kwenye Uwanja wa Boko Veterani uliopo jijini Dar es Salaam leo asubuhi na jioni.
Katika mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar, Simba iliwakosa wachezaji Juuko Murushid, James Kotei na Erasto Nyoni ambao walikuwa wanatumikia adhabu ya kadi 3 za njano kwa kila mmoja.
Tayari wachezaji hao wameshamaliza adhabu hiyo na kesho wanatarajia kuwa sehemu ya kikosi cha wekundu hao wa Msimbazi Simba.
Kocha Msaidizi wa Simba Masoud Djuma ameonekana hana wasiwasi na kikosi chake kuelekea mchezo huo wa kesho ambapo anaamini ushindi ndiyo jambo la msingi ili kupata ubingwa wa msimu huu.
Simba wanaongoza ligi wakiwa na alama 52 wakifuatiwa na mahasimu wao Yanga wenye alama 46 ambapo wanacheza leo dhidi ya Singida.
Hivyo makala SIMBA YAIVUTIA KASI MBEYA CITY, WAENDELEA NA MAZOEZI
yaani makala yote SIMBA YAIVUTIA KASI MBEYA CITY, WAENDELEA NA MAZOEZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SIMBA YAIVUTIA KASI MBEYA CITY, WAENDELEA NA MAZOEZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/simba-yaivutia-kasi-mbeya-city.html
0 Response to "SIMBA YAIVUTIA KASI MBEYA CITY, WAENDELEA NA MAZOEZI"
Post a Comment