title : MAHAKAMA KISUTU YASOGEZA MBELE TAREHE YA KUSOMWA MAELEZO YA AWALI VIGOGO TFF
kiungo : MAHAKAMA KISUTU YASOGEZA MBELE TAREHE YA KUSOMWA MAELEZO YA AWALI VIGOGO TFF
MAHAKAMA KISUTU YASOGEZA MBELE TAREHE YA KUSOMWA MAELEZO YA AWALI VIGOGO TFF
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesogeza mbele tarehe ya kuwasomea maelezo ya awali (PH ) ya vigogo watatu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) hadi Aprili 18/2018.
Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro kuitaarifu Mahakama kuwa wanaomba kufanya mabadiliko ya hati ya mashtaka kwanza ndiyo waendelee na PH.
Wakili Kimaro amedai, "kesi leo imepangwa kwa ajili ya PH, Mimi ndiyo nimepangiwa kuendelea na kesi hii, nimefanya Mawasiliano na (Takukuru) tukapitia ushahidi uliokusanywa hivyo tunaomba kufanya mabadiliko ya hati ya mashtaka Kwa kuongeza washtakiwa wengine ndiyo tuendelee na PH" ameeleza..
Maelezo hayo ya awali leo yalipaswa kusomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.
Kimaro aliendelea kudai kuwa mmoja wa washtakiwa wanaopaswa kuunganishwa kwenye kesi hivyo yupo nje ya Dar es Salaam na utaratibu wa kumleta umekamilika.
Kutokana na taarifa hiyo, Hakimu Mashauri aliiahirisha kesi hiyo hadi Aprili 18 mwaka 2018.
Watuhumiwa katika kesi hiyo ni, aliyekuwa Rais TFF, Jamal Malinzi(57), Katibu Mkuu, Mwesigwa Selestine(46) na Mhasibu, Nsiande Mwanga(27)
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha dola za Marekani 375,418. 7
Katika kesi hiyo, Malinzi na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 28 ya uhujumu uchumi ikiwamo kughushi na utakatishaji wa fedha dola za marekani 375,418.
Hivyo makala MAHAKAMA KISUTU YASOGEZA MBELE TAREHE YA KUSOMWA MAELEZO YA AWALI VIGOGO TFF
yaani makala yote MAHAKAMA KISUTU YASOGEZA MBELE TAREHE YA KUSOMWA MAELEZO YA AWALI VIGOGO TFF Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA KISUTU YASOGEZA MBELE TAREHE YA KUSOMWA MAELEZO YA AWALI VIGOGO TFF mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/mahakama-kisutu-yasogeza-mbele-tarehe.html
0 Response to "MAHAKAMA KISUTU YASOGEZA MBELE TAREHE YA KUSOMWA MAELEZO YA AWALI VIGOGO TFF"
Post a Comment