MSANII DIAMOND KUTOA BURUDANI KOMBE LA DUNIA 2018 NCHINI URUSI

MSANII DIAMOND KUTOA BURUDANI KOMBE LA DUNIA 2018 NCHINI URUSI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MSANII DIAMOND KUTOA BURUDANI KOMBE LA DUNIA 2018 NCHINI URUSI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MSANII DIAMOND KUTOA BURUDANI KOMBE LA DUNIA 2018 NCHINI URUSI
kiungo : MSANII DIAMOND KUTOA BURUDANI KOMBE LA DUNIA 2018 NCHINI URUSI

soma pia


MSANII DIAMOND KUTOA BURUDANI KOMBE LA DUNIA 2018 NCHINI URUSI

Msanii nyota wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Diamond Platnumz, kwa kushirikiana na kampuni ya Coca-Cola ametangaza kuwa ameshiriki kuimba wimbo utakaosherehesha Kombe la Dunia 2018 uitwao Colours. 

Wimbo huo uliotungwa na mwanamuziki Jason Derulo wa Florida, Marekani, Diamond ameshiriki kuweka maudhui ya lugha ya Kiswahili na umetayarishwa na prodyuza Nahreel kwa kushirikiana na maprodyuza kutoka nchi nyingine chini ya udhamini wa kampuni ya Coca-Cola. 

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, amesema anayo furaha kupata fursa ya kushiriki kuimba kuimba wimbo wa mashindano haya makubwa ya kidunia na kuitangaza Tanzania na lugha ya Afrika bila kusahau tasnia ya muziki kwa ujumla. 

“Kwangu hii ni nafasi nyingine ambayo najivunia kuipata ya kutangaza muziki wa kitanzania sambamba na lugha ya Kiswahili kwa kuwa sehemu niliyoshiriki kuimba nimetumia lugha ya taifa la Tanzania ambayo inazidi kupata umaarufu mkubwa duniani”alisema Diamond.

Kwa upande wake Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini, Sialouise Shayo, alisema kampuni ya Coca-Cola ambayo ni moja ya mdhamini wa mashindano haya makubwa ya soka duniani inayo furaha kwa msanii kutoka nchini Tanzania kushiriki kuimba wimbo maalum wa mashindano haya. “Tuna imani Watanzania watapata mzuka wa soka dimbani na kujisikia sehemu ya mashindano haya”alisisitiza. 

Prodyuza nguli wa muziki nchini na kanda ya Afrika Mashariki, Nahreel ,ambaye ameshiriki kutengeneza wimbo huu aliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa jitihada mbalimali ambazo imekuwa ikifanya kuwanyanyua wasanii wa hapa nchini ambapo mbali na Diamond naye ameshiriki kwenye tukio hili kubwa. 
“Ninayo furaha ya kufanya kazi na Diamond kwa mara nyingine katika tukio hili kubwa la mashindano ya Kombe la Dunia na najivunia heshima kubwa tuliyopewa”
 Msanii Diamond akiongea katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es alaam (katikati) ni Sealouise Shayo, Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini (kulia) ni Meneja wake Sallam SK.
 Msanii Diamond na Nahreel katika mkutano wa waandishi wa habari, wengine ni maofisa wa Coca-Cola na mameneja wa msanii Diamond.
Maofisa wa Coca-Cola wakiwa katika picha ya pamoja na Diamond na Nahreel baada ya mkutano na waandishi wa habari.


Hivyo makala MSANII DIAMOND KUTOA BURUDANI KOMBE LA DUNIA 2018 NCHINI URUSI

yaani makala yote MSANII DIAMOND KUTOA BURUDANI KOMBE LA DUNIA 2018 NCHINI URUSI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MSANII DIAMOND KUTOA BURUDANI KOMBE LA DUNIA 2018 NCHINI URUSI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/msanii-diamond-kutoa-burudani-kombe-la.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MSANII DIAMOND KUTOA BURUDANI KOMBE LA DUNIA 2018 NCHINI URUSI"

Post a Comment