title : MHE SAMIA SULUHU AHUDHURIA MKUTANO WA SADC TROIKA EXTRA JIJINI LUANDA, ANGOLA
kiungo : MHE SAMIA SULUHU AHUDHURIA MKUTANO WA SADC TROIKA EXTRA JIJINI LUANDA, ANGOLA
MHE SAMIA SULUHU AHUDHURIA MKUTANO WA SADC TROIKA EXTRA JIJINI LUANDA, ANGOLA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amemuwakilisha Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC aliyemaliza muda wake kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda umefanyika hapa Luanda, leo tarehe 24 Aprili, 2018.
Mkutano huu umeitishwa baada ya mashauriano kati ya Mheshimiwa Dkt. Cyril Ramaphosa, Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini na Mwenyekiti wa SADC na Mhe. João Lourenço, Rais wa Angola na Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikino ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC Mkutano huu umetanguliwa na kikao cha Mawaziri ambacho kilifanyika jana tarehe 23 April 2018.
Mkutano huu ulihusisha nchi wanachama sita tu wa SADC Double Troika na Viongozi wafuatao walihudhuria, Mhe. Dkt. Cyril Ramaphosa, Rais wa Afrika Kusini na Mwenyekiti wa Summit, Mhe. João Lourenço , Rais wa Angola na Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama – (SADC Organ on Politics, Defence and Security Cooperation),Mhe. Hage Geingob, Rais wa Namibia na Makamu Mwenyekiti wa Summit, Mhe. Edgar Lungu, Rais wa Zambia na Makamu Mwenyekiti wa SADC Organ, Mfalme Mswati III, Mfalme wa Swaziland na Mwenyekiti wa Summit anayetoka; Mheshimiwa Joseph Kabila Kabange, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mheshimiwa Thomas Thabane, Waziri Mkuu wa Lesotho walialikwa na walihudhuria.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda, Luanda Angola.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja Wakuu wa Nchi na Serikali muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda, Luanda Angola.
Wengine pichani kutoka kushoto ni Mheshimiwa Thomas Thabane, Waziri Mkuu wa Lesotho Mhe. Edgar Lungu, Rais wa Zambia, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Rais Joseph Kabila, Mfalme Mswati III, Mfalme wa Swaziland Mhe. Dkt. Cyril Ramaphosa Rais wa Afrika Kusini na Mwenyekiti wa Summit, Mhe. João Lourenço Rais wa Angola na Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama – (SADC Organ on Politics, Defence and Security Cooperation), Mhe. Hage Geingob Rais wa Namibia na Makamu Mwenyekiti wa Summit
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifuatilia kwa makini Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda, Luanda Angola. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza mara baada ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda kumalizika mjini Luanda Angola. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Hivyo makala MHE SAMIA SULUHU AHUDHURIA MKUTANO WA SADC TROIKA EXTRA JIJINI LUANDA, ANGOLA
yaani makala yote MHE SAMIA SULUHU AHUDHURIA MKUTANO WA SADC TROIKA EXTRA JIJINI LUANDA, ANGOLA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MHE SAMIA SULUHU AHUDHURIA MKUTANO WA SADC TROIKA EXTRA JIJINI LUANDA, ANGOLA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/mhe-samia-suluhu-ahudhuria-mkutano-wa.html
0 Response to "MHE SAMIA SULUHU AHUDHURIA MKUTANO WA SADC TROIKA EXTRA JIJINI LUANDA, ANGOLA"
Post a Comment