Zoezi la Kuorodhesha Kaya Kwa Ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi Linaendelea Kufanyika Nchini.

Zoezi la Kuorodhesha Kaya Kwa Ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi Linaendelea Kufanyika Nchini. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Zoezi la Kuorodhesha Kaya Kwa Ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi Linaendelea Kufanyika Nchini., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Zoezi la Kuorodhesha Kaya Kwa Ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi Linaendelea Kufanyika Nchini.
kiungo : Zoezi la Kuorodhesha Kaya Kwa Ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi Linaendelea Kufanyika Nchini.

soma pia


Zoezi la Kuorodhesha Kaya Kwa Ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi Linaendelea Kufanyika Nchini.






Na: Veronica Kazimoto
Dar es Salaam
17 Julai, 2017.
ZOEZI la kuorodhesha kaya kwa ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 linaendelea nchi nzima ikiwa ni maandalizi ya utafiti huo unaotarajia kufanyika hivi karibuni.

Akizungumzia zoezi hilo, Meneja wa Takwimu za Jamii na Watu, Sylvia Meku wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu amesema mpaka sasa mikoa kumi na tatu (13) imekamilisha zoezi hilo ambapo ni sawa na silimia 50.

“Zoezi la kuorodhesha kaya kwa ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 linaendelea vizuri na mpaka sasa wadadisi wamekamilisha kuorodhesha kaya katika mikoa 13,” amesema Sylvia Meku.

Ameitaja mikoa iliyokamilisha zoezi la uorodheshaji wa kaya kuwa ni pamoja na Dar es Salaam, Arusha, Manyara, Iringa, Njombe na Morogoro. Mikoa mingine ni Mwanza, Tabora, Katavi, Mbeya, Mara, Kagera na Lindi.

Zoezi la Uorodheshaji wa Kaya linafanyika mikoa yote ya Tanzania Bara na linatarajia kumalizika mwishoni mwa mwezi Julai, 2017.

Utafiti kama huu mara ya mwisho ulifanyika Mwaka 2011/12 ambao ulionesha kuwa asilimia 28.2 ya Watanzania wanaishi chini ya mstari wa Umaskini wa mahitaji ya Msingi.

Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 unafanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango na baadhi ya Wadau wa Maendeleo kwa lengo la kupata viashiria vya kupima hali ya umaskini nchini.


Hivyo makala Zoezi la Kuorodhesha Kaya Kwa Ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi Linaendelea Kufanyika Nchini.

yaani makala yote Zoezi la Kuorodhesha Kaya Kwa Ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi Linaendelea Kufanyika Nchini. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Zoezi la Kuorodhesha Kaya Kwa Ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi Linaendelea Kufanyika Nchini. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/zoezi-la-kuorodhesha-kaya-kwa-ajili-ya_35.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Zoezi la Kuorodhesha Kaya Kwa Ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi Linaendelea Kufanyika Nchini."

Post a Comment