title : MAKONDA AWATAHADHARISHA WALIOTELEKEZA WATOTO, AWAONYA WATAKAOKAIDI WITO WAKE KUKIONA
kiungo : MAKONDA AWATAHADHARISHA WALIOTELEKEZA WATOTO, AWAONYA WATAKAOKAIDI WITO WAKE KUKIONA
MAKONDA AWATAHADHARISHA WALIOTELEKEZA WATOTO, AWAONYA WATAKAOKAIDI WITO WAKE KUKIONA
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewatahadharisha wanaume wanaodhani wanaweza kukaidi wito wa kufika ofisini kwake baada ya kulalamikiwa kutelekeza watoto ambapo amewatumia salamu kwa kuwaambia wasimjaribu wala kupima mamlaka aliyonayo.
Makonda ametoa kauli hiyo wakati wa mahojiano ya kipindi cha tathimini ya mchakato wa kudai haki za watoto waliotelekezwa ambapo amesema tangu Jumatatu zaidi ya 17,000 walifika ofisini kwake na Kati ya hao 4,400 wamesikilizwa.
Aidha Makonda amesema kinachomfariji ni kuona idadi kubwa ya kinababa wanaofika ofisini kwake wanakubali kumlea mtoto ambapo hadi sasa familia 295 zimekubali kuhudumia mtoto na familia 29 zimepima DNA.*
Hata hivyo Makonda amesema baada ya zoezi hilo ataunda tume ya kuangalia changamoto zilizopo katika sheria ya matunzo ya mtoto* kisha kuifikisha kwa waziri husika kwaajili ya kufikishwa Bungeni kwaajili kufanyiwa marekebisho.
Pamoja na hayo Makonda amesema hatoyumbishwa na baadhi ya watu wasiojua uchungu wanaopata kinamama kwa kubeza zoezi hilo kwakuwa yeye ametambua Mateso waliyokuwa wakipata kinamama waliotelekezwa.
Makonda amesema ikitokea mwanamke aliefika ofisini kwake na kumshitaki mwanaume aliezaanae kisha uchunguzi ukafanyika na kubaini udanganyifu mwanaume anayo haki ya kufungua kesi ya kudhalilishwa na afisa ustawi wa jamii wa mkoa atalazimika kuwa shahidi mahakamani.
WATU WENYE DHAMBI WANAPENDA GIZA NDIO MAANA UKIWASHA NURU WANAIBUKA KUPINGA.
Hivyo makala MAKONDA AWATAHADHARISHA WALIOTELEKEZA WATOTO, AWAONYA WATAKAOKAIDI WITO WAKE KUKIONA
yaani makala yote MAKONDA AWATAHADHARISHA WALIOTELEKEZA WATOTO, AWAONYA WATAKAOKAIDI WITO WAKE KUKIONA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKONDA AWATAHADHARISHA WALIOTELEKEZA WATOTO, AWAONYA WATAKAOKAIDI WITO WAKE KUKIONA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/makonda-awatahadharisha-waliotelekeza.html
0 Response to "MAKONDA AWATAHADHARISHA WALIOTELEKEZA WATOTO, AWAONYA WATAKAOKAIDI WITO WAKE KUKIONA"
Post a Comment