title : MAHAKAMA YAELEZWA HALI TETE RAIS WA KLABU YA SIMBA, EVANS AVEVA
kiungo : MAHAKAMA YAELEZWA HALI TETE RAIS WA KLABU YA SIMBA, EVANS AVEVA
MAHAKAMA YAELEZWA HALI TETE RAIS WA KLABU YA SIMBA, EVANS AVEVA
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, hali ya Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva ni mbaya (very Serious), na amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Kufuatia hali hiyo, mahakama imeshindwa kuwasomea maelezo ya awali (PH) rais huyo Simba ambaye anashtakiwa pamoja na makamu wake, Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu.
Kesi imeahirishwa baada ya Mwendesha Mashtaka kutoka Takukuru, Leonard Swai kueleza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa Aveva ni mgonjwa (very Serious) amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Swai aliomba mahakama iipangie kesi hiyo tarehe nyingine wakati wakisubiri afya ya Aveva iimarike.
Hakimu Simba ameutaka upande wa mashtaka kuhakikisha unaandaa maelezo ya awali, ili tarehe inayokuja waweze kusomewa PH na siku ikianza kusikilizwa, isikilizwe mfululizo.
Kesi imeahirishwa hadi Aprili 25/ 2018.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi na kutakatisha fedha dola za kimarekani 300,000.
Hivyo makala MAHAKAMA YAELEZWA HALI TETE RAIS WA KLABU YA SIMBA, EVANS AVEVA
yaani makala yote MAHAKAMA YAELEZWA HALI TETE RAIS WA KLABU YA SIMBA, EVANS AVEVA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA YAELEZWA HALI TETE RAIS WA KLABU YA SIMBA, EVANS AVEVA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/mahakama-yaelezwa-hali-tete-rais-wa.html
0 Response to "MAHAKAMA YAELEZWA HALI TETE RAIS WA KLABU YA SIMBA, EVANS AVEVA"
Post a Comment