KAMISHNA WA NISHATI AFANYA ZIARA KITUO CHA KUPOKEA MAFUTA CHA KURASINI

KAMISHNA WA NISHATI AFANYA ZIARA KITUO CHA KUPOKEA MAFUTA CHA KURASINI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KAMISHNA WA NISHATI AFANYA ZIARA KITUO CHA KUPOKEA MAFUTA CHA KURASINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KAMISHNA WA NISHATI AFANYA ZIARA KITUO CHA KUPOKEA MAFUTA CHA KURASINI
kiungo : KAMISHNA WA NISHATI AFANYA ZIARA KITUO CHA KUPOKEA MAFUTA CHA KURASINI

soma pia


KAMISHNA WA NISHATI AFANYA ZIARA KITUO CHA KUPOKEA MAFUTA CHA KURASINI

Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga alifanya ziara katika kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) kilichopo jijini Dar es Salaam, lengo likiwa ni kukagua shughuli zinazotekelezwa na kituo hicho pamoja na kutatua changamoto mbalimbali. 

Katika ziara hiyo Mhandisi Luoga aliambatana na Kamishna Msaidizi wa Petroli, Mhandisi Mwanamani Kidaya, wataalam kutoka Idara ya Nishati na mwakilishi kutoka Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA).

Kamishna Luoga alielekeza kituo hicho kuendelea kuimarisha ulinzi ili kudhibiti upotevu wa mafuta. Aidha alielekeza kituo hicho kuendelea kushirikiana na wadau wengine kwa karibu zaidi katika kuboresha shughuli zake.
Meneja wa kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) Captain Paul R. Paul (kushoto) akielezea kazi za mita za kupimia mafuta (flow meters) katika kituo hicho kwa Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (kulia)
Meneja wa kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) Captain Paul R. Paul (katikati mbele) Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (kushoto mbele) na Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Masuala ya Petroli, Mhandisi Mwanamani Kidaya (kulia mbele) wakiendelea na ziara katika kituo hicho.
Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (katikati) akielekeza jambo katika sehemu ya kupokea mafuta aina ya petroli na dizeli katika kituo hicho.
Meneja wa kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) Captain Paul R. Paul (mbele) akimwongoza Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Masuala ya Petroli, Mhandisi Mwanamani Kidaya pamoja na wajumbe wengine katika ziara hiyo.
Sehemu ya gati za kupokea mafuta katika kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam.
Meneja wa kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) Captain Paul R. Paul (katikati) akionesha sehemu ya mita za kupima mafuta (flow meters) katika kituo hicho kwa Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (kushoto) pamoja na wajumbe wengine (hawapo pichani) katika ziara hiyo.


Hivyo makala KAMISHNA WA NISHATI AFANYA ZIARA KITUO CHA KUPOKEA MAFUTA CHA KURASINI

yaani makala yote KAMISHNA WA NISHATI AFANYA ZIARA KITUO CHA KUPOKEA MAFUTA CHA KURASINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KAMISHNA WA NISHATI AFANYA ZIARA KITUO CHA KUPOKEA MAFUTA CHA KURASINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/kamishna-wa-nishati-afanya-ziara-kituo.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "KAMISHNA WA NISHATI AFANYA ZIARA KITUO CHA KUPOKEA MAFUTA CHA KURASINI"

Post a Comment