title : KAMPUNI YA TECNO TANZANIA YAMPA UBALOZI GABO
kiungo : KAMPUNI YA TECNO TANZANIA YAMPA UBALOZI GABO
KAMPUNI YA TECNO TANZANIA YAMPA UBALOZI GABO
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
MUGIZAJI wa filamu za kibongo nchini Salim Ahmed a.k.a Gabo, ametangazwa kuwa balozi wa simu mpya ya mkononi kutoka Kampuni ya Tecno Tanzania iliyopewa jina la Tecno Pop 1 ambayo itauzwa kwenye maduka yote ya Vodashop nchini.
Akizungumza Dar es Salaam wakati wa kumtangaza Gabo kuwa balozi wa simu hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Biashara na ushirikiano wa Tecno,Anuj Khosla amesem wameamua kuileta simu hiyo ili kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini kumiliki simu janja .
"Tuna furaha kubwa kuwatangazia uwepo wa simu hii ambayo mtu akinunua atapata na GB 10 kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ili kuperuzi mtandao na kujielimisha kupitia simu hii janja ambayo ina uwezo mkubwa,"amesema Khosla
Kwa upande wake Gabo amesema anaishukuru Tecno kwa kumpa nafasi hiyo ya kufungua njia kuwa balozi kwani ndio ubalozi wa kwanza kuupata tangu aanze kujulikana katika tasnia ya filamu.
"Naamini huu ndio mwanzo wa mimi kuendelea kufanya kazi na kampuni kubwa baada ya hii kampuni ya simu kuniona Gabo na kunifanya kuwa balozi wa kutangaza bidhaa zao.Ni jambo jema ambalo kila msanii anatamani kulifikia ukiacha mafanikio ya sanaa ya kawaida,"amesema Gabo.
Amesema kwa sasa yeye kama msanii mkubwa anatumia nafasi hiyo kufikisha ujumbe kwa mashabiki na kuwataka watumie simu hizo ambazo zina ubora na bei nafuu mpaka kwa watanzania wa kawaida.
Mkuu wa kitengo cha Biashara na ushirikiano wa Tecno, Anuj Khosla akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa Simu mpya ya Tecno POP 1 itakayotolewa na GB 10 za Vodacom leo Jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Filamu wa nchini, Salim Ahmed "Gabo", akionyesha simu aina ya Tecno POP inayotolewa na GB 10 Za Vodacom. kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha manunuzi ya rejareja ya simu kutoka Vodacom, Brigita Stephene.
Msanii wa Filamu wa nchini Salim Ahmed "Gabo" akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Vodacom na Tecno Tanzania.Hivyo makala KAMPUNI YA TECNO TANZANIA YAMPA UBALOZI GABO
yaani makala yote KAMPUNI YA TECNO TANZANIA YAMPA UBALOZI GABO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMPUNI YA TECNO TANZANIA YAMPA UBALOZI GABO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/kampuni-ya-tecno-tanzania-yampa-ubalozi.html
0 Response to "KAMPUNI YA TECNO TANZANIA YAMPA UBALOZI GABO"
Post a Comment