title : Basata kutoa tuzo kwa wanafunzi wa Sekondari hapa nchini
kiungo : Basata kutoa tuzo kwa wanafunzi wa Sekondari hapa nchini
Basata kutoa tuzo kwa wanafunzi wa Sekondari hapa nchini
Na Agness Francis,Blogu ya Jamii
BARAZA la sanaa Taifa (BASATA) lenye dhamana ya kufufua kukuza na kuendesha sekta ya sanaa kutoa tuzo kwa wanafunzi wa kidato cha 4 kwa shule 5 za Sekondari waliofanya vizuri masoma ya sanaa hapa nchini.
Shule hizo zitakazo husika katika kupewa tuzo hizo ni Mbeya Sekondari wanafunzi 2,Dodoma Sekondari 1,Edmund-Recesinon Sekondari Arusha 1,Mvuha Sekondari Morogoro 1 pamoja na Murungwa sekondari Kagera 2.
Baraza hilo limeamua kufufua programu endelevu ya utoaji wa tuzo kwa wanafunzi wa shule za sekondari waliofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha 4 kwa mujibu wa sheria namba 23 mwaka 1984.
Ambapo safari hii watatoa kwa wanafunzi waliomaliza mwaka 2016 na kufaulu katika masomo ya sanaa za ufundi,maonyesho na muziki.
Aidha amezungumza na wandishi wa habari katika ofisi zake basata Jijini Dar Es Salaam mkurugenzi wa masoko na ukuzaji sanaa Basata Vivian Shalua amesema kuwa utoaji wa tuzo hizo itachochea wanafunzi wengi kusoma masomo hayo katika kazi za sanaa na kuwasaidia kuongeza ufaulu wao darasani hasa ukizingatia sanaa ni nyenzo katika kumuandaa mtoto kielimu na kimaadili.
"Sanaa ni chanzo cha ajira kwa vijana wengi ambao wameweza kijipa kipato na umaarufu kupitia fani hizi za Sanaa,hata hivyo masomo haya yamekuwa hayapatiwi kipaumbele kama yalivyo masomo mengine katika shule za msingi na sekondari"amesema Mama Shalua.
Mama shalua ametoa wito kwa kuwaalika wadau wote wa sanaa hapa nchini kufika kushuhudia utoaji wa tuzo hizo ambazo kauli mbiu yake (sanaa ni kazi ,nchi yangu kwanza).
Tuzo hizo zitatolewa Aprili 28 mwaka huu saa 4 asubui katika ukumbi wa Basata Sharifushamba Ilala Jijini Dar Es Salaam.
Hivyo makala Basata kutoa tuzo kwa wanafunzi wa Sekondari hapa nchini
yaani makala yote Basata kutoa tuzo kwa wanafunzi wa Sekondari hapa nchini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Basata kutoa tuzo kwa wanafunzi wa Sekondari hapa nchini mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/basata-kutoa-tuzo-kwa-wanafunzi-wa.html
0 Response to "Basata kutoa tuzo kwa wanafunzi wa Sekondari hapa nchini"
Post a Comment