WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA MRADI WA UJENZI WA ‘TERMINAL III’

WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA MRADI WA UJENZI WA ‘TERMINAL III’ - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA MRADI WA UJENZI WA ‘TERMINAL III’, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA MRADI WA UJENZI WA ‘TERMINAL III’
kiungo : WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA MRADI WA UJENZI WA ‘TERMINAL III’

soma pia


WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA MRADI WA UJENZI WA ‘TERMINAL III’

Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa.  Katikati  mwenye tai akikagua maendeleo ya ujenzi  wa Jengo la Tatu la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa  wa   Julius Nyerere (JNIA), Jijini Dar es Salaam,leo March 23/2018 .Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Paul Makonda na kulia ni Msimamizi wa Mradi. Eng. Julius Ndyamukama.
 Mwonekano wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na kwamba ameridhishwa na maendeleo yake.

Mradi wa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika Juni 2019 na utakuwa na uwezo wa kuegesha ndege kubwa 24 kwa wakati mmoja, pamoja na kuhudumia abiria milioni sita kwa mwaka na kuwa na.

Waziri Mkuu ambaye ametembelea mradi huo leo (Ijumaa, Machi 23, 2018) amesema amefarijika na maendeleo ya ujenzi wa mradi huo pamoja na kukuta Watanzania wengi wakishiriki katika kazi za ujenzi.

“Serikali imejiimarisha katika kuboresha usafiri wa anga, ambapo kukamilika kwa jengo hili kutachangia ongezeko la ndege kubwa nyingi kutua nchini. Pia sekta ya utalii nayo itaimarika kwa kuwa watalii wanaoingia nchini wataongezeka.”

Amesema mbali na ujenzi wa jengo hilo, pia Serikali inaendelea kuvikarabati viwanja mbalimbali vya ndege nchini kikiwemo cha Musoma, Iringa, Kilwa Masoko, Lake Manyara, Lindi, Moshi, Njombe, Tanga, Simiyu, Singida na Songea ili kuboresha huduma za usafiri wa anga nchini.
Akisoma taarifa za ujenzi wa mradi Mkurugenzi wa Miradi wa TANROADS, Mhandisi Christianus Ako amesema mradi huo umeajiri wafanyakazi 1,400 kwa sasa na wanatarajia kuongeza watumishi na kufikia 1,800.

Pia wanatarajia kufanya majaribio ya kwanza ya mifumo na vifaa vya umeme kuanzia Julai, 2018 kwa kuwa tayari utekelezaji wa kazi kubwa za ujenzi wa mradi huo zimefanyika.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, MACHI 23, 2018.


Hivyo makala WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA MRADI WA UJENZI WA ‘TERMINAL III’

yaani makala yote WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA MRADI WA UJENZI WA ‘TERMINAL III’ Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA MRADI WA UJENZI WA ‘TERMINAL III’ mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/waziri-mkuu-aridhishwa-na-mradi-wa_24.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA MRADI WA UJENZI WA ‘TERMINAL III’"

Post a Comment