SERIKALI YATANGAZA KUTOA BINGO KWA WATAKAOSAIDIA KUWAFICHUA WEZI WA ALAMA ZA BARABARANI

SERIKALI YATANGAZA KUTOA BINGO KWA WATAKAOSAIDIA KUWAFICHUA WEZI WA ALAMA ZA BARABARANI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YATANGAZA KUTOA BINGO KWA WATAKAOSAIDIA KUWAFICHUA WEZI WA ALAMA ZA BARABARANI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YATANGAZA KUTOA BINGO KWA WATAKAOSAIDIA KUWAFICHUA WEZI WA ALAMA ZA BARABARANI
kiungo : SERIKALI YATANGAZA KUTOA BINGO KWA WATAKAOSAIDIA KUWAFICHUA WEZI WA ALAMA ZA BARABARANI

soma pia


SERIKALI YATANGAZA KUTOA BINGO KWA WATAKAOSAIDIA KUWAFICHUA WEZI WA ALAMA ZA BARABARANI

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa(kushoto)  akitoa maelekezo jana katika eneo la Nyahua wilayani Uyui  kwa Mwakilishi wa Kampuni ya CHICO  Peng Hao (kulia) mara baada ya kutembelea eneo la barabara ya Itigi hadi Tabora lililoharibiwa na maji ya mvua.
Picha na Tiganya Vincent
………………..
NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
SERIKALI imetangaza kutoa zawadi nomo kwa wananchi watakaosaidia kutoa taarifa za siri za kuwafichua watu wanaong’oa alama za barabarani na kuisababishia hasara kutokana na urejeshaji wake.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa  mara baada ya kukagua ukarabati wa eneo Nyahua ambalo lilikuwa limekatika kutokana na maji ya mvua yaliyopelekea kukosekana kwa mawasiliano baina ya Itigi na Tabora jana wilayani Uyui.
Alisema Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuweka alama za barabara ili kuwaongoza watumiaji wa barabara kuepuka ajali lakini baadhi ya watu wamekuwa wakihuju na kung’oa alama hizo kwa ajili ya kwenda kuziua kama vyuma chakavu.
Kwandikwa alisema mtu atakayesaidia kutoa siri ya wanaong’oa alama hizo na wanunuzi wake atapewa zawadi na jina lake halitafichuliwa kwa ajili ya usalama wake.
Alisema inasikitisha kuona kuwa alama zipatazo 78 zenye thamani ya shilingi milioni 27 katika kipande cha barabara ya urefu kilometa zipatazo 80.6 kutoka Tabora hadi Nyahua zimeng’olewa.
Naibu Waziri huyo alisema alama hizo zinatumia fedha nyingi za Serikali kwa kuwa baadhi yake zinatoka nje ya nchi na kuongeza kuwa vitendo hivyo ni hatari sana ni vema wahusika wakikamatwa washitakiwe kama wahujumu uchumi.
Alisema hata pale Serikali ilipoamua kujengwa alama hizo kwa Sementi bado baadhi ya watu wamekuwa wakizivunja ili kutoa nondo zilitumika katika ujenzi wake.
“Fikiria katika muda wa siku moja alama zaidi ya moja alama za barabarani 30 mkoani Kilimanjaro zimeng’olewa … Je? Kwa mwezi ni alama ngapi zinang’olewa ..pesa ngapi za Serikali inapotea kurudisha alama hizo …Ma RC na Ma DC na wananchi saidieni katika kupambana na wahujumu wa miundombinu katika maeneo yenu” alisema Kwandikwa.
Aidha Naibu Waziri huyo alisema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wauzaji na wanunuzi wa vyuma chakavu watakoa patikana na alama za barabara ili iwe fundisho kwa watu wanohujumu miundimbinu.
Kwandikwa alisema jamii inawajua vema wanaonunua vyuma chakavu ni vema wakatoa taarifa za siri ili kukomesha tatizo hilo ambalo limekuwa likichangia sehemu ya ajali nyingine za barabarani.
“Meneja wa TANROADS nafikiri tuanze kutoa kiasi fulani cha fedha kwa mtu anayetusaidia kutoa taarifa za siri kwa watu wanaong’oa alama za barabarani ili tukomesha tatizo” alisema Naibu Waziri.
Hivi karibuni Kamati ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa katika ziara yake ya kikazi Mkoani Tabora ilielezea kusikitishwa kwake na wizi wa alama za barabarani katika barabara nyingi za Mkoa huo na kuagiza viongozi wa maeneo husika ambapo barabara kuu zinapita wasimamie ulinzi.


Hivyo makala SERIKALI YATANGAZA KUTOA BINGO KWA WATAKAOSAIDIA KUWAFICHUA WEZI WA ALAMA ZA BARABARANI

yaani makala yote SERIKALI YATANGAZA KUTOA BINGO KWA WATAKAOSAIDIA KUWAFICHUA WEZI WA ALAMA ZA BARABARANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YATANGAZA KUTOA BINGO KWA WATAKAOSAIDIA KUWAFICHUA WEZI WA ALAMA ZA BARABARANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/serikali-yatangaza-kutoa-bingo-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI YATANGAZA KUTOA BINGO KWA WATAKAOSAIDIA KUWAFICHUA WEZI WA ALAMA ZA BARABARANI"

Post a Comment