title : Waziri Dkt. Kalemani ateua Wahandisi 7 Kusimamia REAIII
kiungo : Waziri Dkt. Kalemani ateua Wahandisi 7 Kusimamia REAIII
Waziri Dkt. Kalemani ateua Wahandisi 7 Kusimamia REAIII
Na Zuena Msuya, Dodoma.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amewateua Wahandisi Saba(7) kutoka Wizara ya Nishati watakaoshirikiana na wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa REA III katika kila Kanda ili kuboresha na kurahisisha utekelezaji wa Mradi huo kwa ufanisi.
Dkt. Kalemani alifanya uteuzi huo baada ya kufanya mkutano na Wadau mbalimbali wanaotekeleza Mradi wa REA III wakiwemo, Wakandarasi, Wawekezaji wenye Viwanda vya kutengeneza miundombinu ya umeme kama vile Trasfoma, Mita, pamoja na nyaya za umeme , Mameneja wa Kanda, na Wahandisi wanaosimamia Mradi ya REA III nchi nzima.
Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina ulipo Makao Makuu ya Nchi Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine ulilenga kujadili hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu pamoja na changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa Mradi huo.
Dkt.Kalenani alisema Wahandisi walioteuliwa watashirikiana na Wakandarasi wa REA III kutafanya kazi mbalimbali pamoja na kuwa na mpango kazi wa kila wiki wa kila Mkandarasi katika eneo husika ili kusisimamia kwa ukaribu utekelezaji wake.
Pia watarahisisha mawasiliano yamoja kwa moja kutoka kwa wakandarasi hao na Wizara ya Nishati ili kufahamu hatua waliofikia na changamoto watakazokuwa wakikabiliana nazo kwa Lengo la kuzitafutia ufumbuzi wa haraka.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani( katikati) na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ( kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamis Mwinyimvua( kulia) wakisikiliza maoni ya wadau wanaotekeleza mradi wa REA III katika ukumbi wa hazina wakati wa mkutano wa wadau hao uliofanyika mkoani Dodoma.
Washiriki wa mkutano wa wadau wakiwa kwenye mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa hazina Mkoani Dodoma.
Watendaji wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake wakimsikiliza waziri wa nishati Dkt. Medard Kalemani( hayupo pichani) akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wanaotekeleza mradi wa REA III uliofanyika katika ukumbi wa hazina Mkoani Dodoma.
Hivyo makala Waziri Dkt. Kalemani ateua Wahandisi 7 Kusimamia REAIII
yaani makala yote Waziri Dkt. Kalemani ateua Wahandisi 7 Kusimamia REAIII Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waziri Dkt. Kalemani ateua Wahandisi 7 Kusimamia REAIII mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/waziri-dkt-kalemani-ateua-wahandisi-7.html
0 Response to "Waziri Dkt. Kalemani ateua Wahandisi 7 Kusimamia REAIII"
Post a Comment