title : UMOJA WA MATAIFA YAIMWAGIA SIFA JWTZ NA SERIKALI YA JPM
kiungo : UMOJA WA MATAIFA YAIMWAGIA SIFA JWTZ NA SERIKALI YA JPM
UMOJA WA MATAIFA YAIMWAGIA SIFA JWTZ NA SERIKALI YA JPM
Mwakilishi maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia watoto na Migogoro ya Kivita Virginia Gamba akizungumza na Meja Afred Mwinuka wakati alipotembelea kambi ya Wanajeshi kutoka jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaoshiriki Ulinzi wa Amani chini ya Mpango wa umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID Shangilitobaya Jimboni Darfur Nchini Sudan ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Msafara Wanajeshi kutoka jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaoshiriki Ulinzi wa Amani chini ya Mpango wa umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID wakiwa katika Doria maeneo ya kijiji cha Shardai Jimboni Darfur Nchini Sudan ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Na Luteni Selemani Semunyu, UNAMID
Umoja wa mataifa UN umeipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais John Magufuli na Mkuu wake wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo kufuatia jitihada zao za kudumisha amani ndani na Nje ya Nchi hiyo.
Hayo yalibainishwa na mwakilishi Malum wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Watoto (Special Representative of Secretary general of Child Abuse and AA) Profesa Virginia Gamba wakati wa Ziara yake kikazi katika Maeneo ya vjiji vya Shangilitobaya Jimboni Darfur nchini Sudan hivi Karibuni.
Alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi ya kuigwa Afrika zinazopiga hatua kubwa ya maendeleo zinazopaswa kutiliwa mfano lakini yote hiyo inatokana na umadhubuti wa Serikali yake, na Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa mchango wake katika kushughulikia mambo ya msingi katika kudumisha Amani.
“Sina budi kuipongeza Serikali chini ya rais John Magufuli inafanya kazi nzuri na Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo kwani utendaji wao ni wa kutukuka Afrika nzima katika kuleta Amani kwani bila Amani hakuna maendeleo hivyo maendeleo yanayotarjiwa Tanzania ytapatikana kwa sababu ya Amani” Alisema Profesa Virginia.
Aliongeza kuwa kutokana na kuimarika kwa Amani ni rahisi kwa nchi yeyote kujiletea maendeleo haraka na kuwataka kuendeleza jitihada hizo kwa kuwalinda watoto ambao ni nusu ya Idadi ya watu Duniani hivyo wakilindwa Watoto Dunia itakuwa salama.
“ Najivunia Tanzania naweza kujiita mi ni rafiki wa Tanzania sio kwa sababu nyingine ni kutokana na Umahiri wao katika Amani ikiwemo jeshi lake la Ulinzi limekuwa Msaada mkubwa katika kuleta Amani kupitia Umoja wa Mataifa” Alisema Profesa Virginia.
Wanajeshi kutoka jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaoshiriki Ulinzi wa Amani chini ya Mpango wa umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID wakiwa katika Doria maeneo ya Jirani na Mlima Mawe Khor Abeche Jimboni Darfur Nchini Sudan ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Hivyo makala UMOJA WA MATAIFA YAIMWAGIA SIFA JWTZ NA SERIKALI YA JPM
yaani makala yote UMOJA WA MATAIFA YAIMWAGIA SIFA JWTZ NA SERIKALI YA JPM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UMOJA WA MATAIFA YAIMWAGIA SIFA JWTZ NA SERIKALI YA JPM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/umoja-wa-mataifa-yaimwagia-sifa-jwtz-na_5.html
0 Response to "UMOJA WA MATAIFA YAIMWAGIA SIFA JWTZ NA SERIKALI YA JPM"
Post a Comment