title : WAKAZI WA MKOA WA DAR ES SALAAM KUPATA MAJI YA KUTOSHA
kiungo : WAKAZI WA MKOA WA DAR ES SALAAM KUPATA MAJI YA KUTOSHA
WAKAZI WA MKOA WA DAR ES SALAAM KUPATA MAJI YA KUTOSHA

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam Kisare Makori amehitimisha maadhimisho ya Wiki ya maji yenye kauli mbiu ya Hifadhi Maji na Mifumo ya Ekolojia kwa Maendeleo ya Jamii.
Akizungumza leo march 22 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Makori amesema maji yanayopatikana jijini kwa sasa ni asilimia 75 pekee na hadi kufikia mwaka 2020 maji yatapatikana kwa asilimia 95 na kufikia mwaka 2025 wakazi wote wa jiji watapata maji kwa asilimia 100.
Aidha Makori ameeleza kuhusu mafanikio ya miradi maji na kusema miradi inayotekelezwa na DAWASA na DAWASCO katika mradi wa Ruvu chini ni lita milioni 270 kutoka lita milioni 182 zinazalishwa kwa siku na kuhudumia wakazi wa Bagamoyo, Kawe na maeneo ya jirani na mradi wa Ruvu juu lita 196 kutoka lita milioni 82 zinazalishwa kwa siku na kuhudumia wakazi wa maeneo ya Kibaha, Mbezi, Ubungo na maeneo ya jirani.
Ameonga kuwa zaidi ya visima 20 vimechimbwa na kunufaisha wakazi wa Kimbiji Mpera na maeneo yake.Amepongezwa wananchi kwa kukubali kuunganishwa na huduma ya maji kutoka laki 123,000 hadi kufikia 228,000.Pia amewataka wananchi kushiriki shughuli za usafi licha ya kuwa na asilimia 10 tu ya wakazi wanaopata huduma hiyo na amehaidi hadi kufikia 2020 asilimia 30 ya wakazi watafikiwa na huduma hiyo.
Hivyo makala WAKAZI WA MKOA WA DAR ES SALAAM KUPATA MAJI YA KUTOSHA
yaani makala yote WAKAZI WA MKOA WA DAR ES SALAAM KUPATA MAJI YA KUTOSHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAKAZI WA MKOA WA DAR ES SALAAM KUPATA MAJI YA KUTOSHA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/wakazi-wa-mkoa-wa-dar-es-salaam-kupata.html
0 Response to "WAKAZI WA MKOA WA DAR ES SALAAM KUPATA MAJI YA KUTOSHA"
Post a Comment