Mimba na ndoa za utotoni zafinya fursa ya mtoto

Mimba na ndoa za utotoni zafinya fursa ya mtoto - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mimba na ndoa za utotoni zafinya fursa ya mtoto, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mimba na ndoa za utotoni zafinya fursa ya mtoto
kiungo : Mimba na ndoa za utotoni zafinya fursa ya mtoto

soma pia


Mimba na ndoa za utotoni zafinya fursa ya mtoto




Na Anthony Ishengoma--Tanga 

Hali ya mimba za utotoni hapa Nchini imeendelea kuongezeka na kumnyima fursa mtoto kike kupata haki yake ya msingi kuendelezwa.

Akiongea na wanafunzi kutoka shule sita za jiji la Tanga katika washa ya siku moja kwa wanafunzi hao kuhusu kampeni ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto Bwana Mathias Haule amesema Elimu ndio njia sahihi kutimiza ndoto za mtoto wa kike. 





Bwana  Haule ameongeza kuwa kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia zinaonesha kuwa jumla ya Wanafunzi 5,053 wameacha shule hapa Nchini kwa ajili ya mimba za utotoni.

Ametaja kuwa mimba 4,426 kwa mujibu wa takwimu hizo kuwa ni kutoka shule za Sekondari na 627 ni kutoka   shule za Msingi, takwimu hizi ni za mwaka 2016.

Aidha ameitaja Mikoa ya Mbeya(380) Mwanza(372), Kilimanjaro(348), Dodoma(308), na Ruvuma(300) kuwa na idadi kubwa za wasichana walioacha shule kwa sababu ya mimba.

Aidha Bw.Haule ameongeza kuwa serikari imebaini sababu za mimba mashuleni ni kuwa ni pamoja na uelewa mdogo wa jamii kuhusu malezi chanya,umuhimu wa mtoto kike kusoma, mila na desturi na umasikini wa familia.

Wakati huo huo Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Tanga Bi.Mwatumu Dossi amesema kwa mwaka 2017 jumla ya wanafunzi wa sekondari 20 walipata ujauzito.

Ametoa wito kwa wazazi na walezi wa Jiji la Tanga kuwa karibu na watoto wao ili kuwapatia elimu ya Afya na jinsia ikiwemo kuacha kuwaoza wasichana katika umri mdogo.

Shule zilizo shiriki kampeni ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni ni shule za msingi za jiji la Tanga ambazo ni Shule ya Msingi Changa,Juhudi,Chumbageni,
Kisosora na shule binafsi ya Changa English Medium.



Hivyo makala Mimba na ndoa za utotoni zafinya fursa ya mtoto

yaani makala yote Mimba na ndoa za utotoni zafinya fursa ya mtoto Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mimba na ndoa za utotoni zafinya fursa ya mtoto mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/mimba-na-ndoa-za-utotoni-zafinya-fursa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Mimba na ndoa za utotoni zafinya fursa ya mtoto"

Post a Comment