title : Uongozi wa Singida United wakanusha kufungiwa kwa Lyanga.
kiungo : Uongozi wa Singida United wakanusha kufungiwa kwa Lyanga.
Uongozi wa Singida United wakanusha kufungiwa kwa Lyanga.
Na Agness Francis, Globu ya jamii
UONGOZI wa Singida United umekana kufungiwa kwa mchezaji wa timu yao Danny Lyanga kwa kosa la kusaini mikataba timu mbili.
Taarifa zilizoenekana kupitia kwa vyombo mbalimbali vya habari, ikielezea kuwa Lyanga amefungiwa na Shirikisho la Mpira duniani (FIFA) kutokana na kudaiwa kusaini kuzitumikia timu mbili ambazo ni Singida United na Fanja Fc ya Oman.
Hivyo FIFA na kuamua kumfungia mchezaji huyo Danny Lyanga kwa muda wa miezi sita kwa kosa la kusaini mkataba timu mbili. Ambapo inasemekana kuwa alisaini mkataba na Singida United wakati wa dirisha dogo akiwa bado ana mkataba wa miaka miwili na klabu ya Fanja FC ya Oman.
Hata hivyo uongozi wa Singinda United umekananusha uvumi huo na kusema si kweli.Umefafanua Lyanga ni mchezaji wao halali wamemsajili kutoka Fanja Fc ya Oman na kufanya makubaliano ya mkataba ambao ulionyesha kuwa mchezaji huo ameshamalizana na kikosi hicho na kuwa huru kununuliwa na Timu nyingine.
Imeelezwamchezaji hiyo hajafungiwa na FIFA miezi 6 kama inavyodaiwa. Kilichotokea mpaka kupelekea uvumi huo kusambaa katika vyombo mbalimbali vya habari ni kuchelewa kupata kibali cha kuchezea nje ya Nchi (ITC) kutoka Fanya Fc.
"Kilichotokea ni kwamba ITC ya Danny Lyanga iljchelewa kuja kutokana na dirisha la usajili kufungwa, hivyo FIFA walituandikia barua sisi pamoja na TFF kwamba ITC ya Lyanga itakamiIika hadi hapo dirisha kubwa la usajiri litakapofunguliwa hapa Tanzania kuanzia Julai 2018.
"Hivyo basi Danny Lyanga hajafungiwa na hivi tunategemea kumtumia kwenye Michuano ambayo klabu yetu itakwenda kushiriki nje ya Nchi"amesema msemaji wa uongozi huo.Uongozi umesema "Tunaomba vyombo vya habari kutumia taarifa rasmi kutoka vyanzo rasmi kwa ajili ya maslai ya Mpira wa miguu hapa nchini".
Hivyo makala Uongozi wa Singida United wakanusha kufungiwa kwa Lyanga.
yaani makala yote Uongozi wa Singida United wakanusha kufungiwa kwa Lyanga. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Uongozi wa Singida United wakanusha kufungiwa kwa Lyanga. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/uongozi-wa-singida-united-wakanusha.html

0 Response to "Uongozi wa Singida United wakanusha kufungiwa kwa Lyanga."
Post a Comment