title : TCCIA KUWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA KUJADILI FURSA ZA MAENDELE
kiungo : TCCIA KUWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA KUJADILI FURSA ZA MAENDELE
TCCIA KUWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA KUJADILI FURSA ZA MAENDELE
Chemba ya biashara, viwanda na kilimo (TCCIA) mwezi huu imeandaa mkutano wa wanachama wake pamoja na wafanyabiashara kwa ujumla. Mkutano huu ambao umebatizwa jiina la TCCIA breakfast utajadili mambo kadhaa ikiwemo; Urahisishaji wa biashara za kimataifa kupitia Benki, Fursa zitokanazo na makubaliano kati ya TCCIA na Chemba ya China, Fursa katika biashara ya bomba la mafuta na pia uboreshaji wa mazingira ya biashara.
Akizungumzia mkutano huo Afisa Mkuu wa TCCIA Gotfrid Muganda alisema " huu ni mwendelezo wa ujengaji uwezo na kuwapa fursa wanachama wake na wafanyabiashara wa Tanzania". Pia TCCIA inalenga kurahisisha ufanyaji wa biashara kati ya China na Tanzania unaolenga kuondoa kabisa utapeli ambao baadhi ya wafanyabiashara wanakumbana nao. Mwaka jana TCCIA ilifanya mikutano kama hiyo mingi kwa mafanikio.
Pia Leo hii Afisa Mtendaji Mkuu wa TCCIA Ndugu Muganda alikutana na mwambata wa ubalozi wa Algeria Nchini Tanzania na kuzungumzia ushirikiano kati ya Tanzania na Algeria. Kupitia mkutano huo Ubalozi wa Algeria umetoa mwaliko wa maonyesho ya kibiashara Nchini Algeria yaitwayo Algeria International Fair mwezi wa tano Mwaka 2018. Mkutano wa breakfast umedhaminiwa na Azania Bank, Air Tanzania na Zurich Insurance
Hivyo makala TCCIA KUWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA KUJADILI FURSA ZA MAENDELE
yaani makala yote TCCIA KUWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA KUJADILI FURSA ZA MAENDELE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TCCIA KUWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA KUJADILI FURSA ZA MAENDELE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/tccia-kuwakutanisha-wafanyabiashara.html
0 Response to "TCCIA KUWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA KUJADILI FURSA ZA MAENDELE"
Post a Comment