title : Serikali yapigia chepuo Program ya Via: Jiandalie Ajira
kiungo : Serikali yapigia chepuo Program ya Via: Jiandalie Ajira
Serikali yapigia chepuo Program ya Via: Jiandalie Ajira
Serikali imesema program ya Via:Jiandalie Ajira ina mchango mkubwa hapa nchini katika kuwajengea vijana ujuzi ambao unawasaidia kujiajiri na kuajiriwa na hiyo ni moja ya harakati za kufikia uchumi wa viwanda na wa kati..
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknilojia, Dkt. Leonard Akwilapo alisema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati alipokuwa akifungua mkutano wa washirika na wadau wa program ya Via: Jiandalie Ajira kuwa program hiyo itasaidia vijana kupata ujuzi utakaowasaidia kujiajiri au kuajiriwa na hiyo ni moja ya harakati za kufikia uchumi wa viwanda na wa kati.
“Sisi katika serikali tunaunga mkono program hii ambayo inatusaidia kutatua tatizo la ajira nchini kwa sababu inawapa fursa vijana kujiajiri na kuajiriwa,” alisema Dkt. Akwilapo.
Program hiyo inatekelezwa na Taasisi ya Kimataifa ya Kuendeleza Vijana Kibiashara (IYF) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya The Mastercard Foundation, Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani (TECC) na Mamlaka ya ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kuwasaidia vijana kupata ujuzi na mafunzo ya ujasiriamali kukabili tatizo la ajira kwa vijana.
Alisema kwamba program hii ina mchango mkubwa sana nchini katika jitihada zake za kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, kwahiyo mkutano huu wa siku saba utatoa fursa ya mjadala, uzoefu kwa vijana waliopata mafunzo hayo na kupata nafasi ya kupitia utekelezaji wake.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa taasisi Taasisi ya Kimataifa ya Kuendeleza Vijana Kibiashara (IYF),Bw. William Reese, akifafanua jambo wakati wa mkutano wa washirika na wadau wa program ya Via: Jiandalie Ajira. Ambapo program hiyo nchini inatekelezwa na IYF kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya The Mastercard Foundation, wake Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani (TECC) na Mamlaka ya ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kuwasaidia vijana kupata ujuzi na mafunzo ya ujasiriamali kukabili tatizo la ajira kwa vijana.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Kuendeleza Vijana Kibiashara (IYF) Bw. William Reese (kulia) akifuatilia mada baada ya kufungua mkutano wa washirika na wadau wa program ya Via: Jiandalie Ajira. Ambapo program hiyo nchini inatekelezwa na IYF kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya The Mastercard Foundation, wake Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani (TECC) na Mamlaka ya ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kuwasaidia vijana kupata ujuzi na mafunzo ya ujasiriamali kukabili tatizo la ajira kwa vijana, (katikati) ni Mwenyekiti wa Bodi ya TECC, Bi. Beng’i Issa, kushoto Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Bw. Dkt. Bwire Ndazi na wengine ni washiriki wa mkutano huo.
Wadau wa Taasisi ya Kimataifa ya Kuendeleza Vijana Kibiashara (IYF) wakifuatilia mada katika mkutano wa washirika na wadau wa program ya Via: Jiandalie Ajira. Ambapo program hiyo nchini inatekelezwa na IYF kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya The Mastercard Foundation, wake Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani (TECC) na Mamlaka ya ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kuwasaidia vijana kupata ujuzi na mafunzo ya ujasiriamali kukabili tatizo la ajira kwa vijana.
Hivyo makala Serikali yapigia chepuo Program ya Via: Jiandalie Ajira
yaani makala yote Serikali yapigia chepuo Program ya Via: Jiandalie Ajira Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Serikali yapigia chepuo Program ya Via: Jiandalie Ajira mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/serikali-yapigia-chepuo-program-ya-via.html
0 Response to "Serikali yapigia chepuo Program ya Via: Jiandalie Ajira"
Post a Comment