Mvua yakata mawasiliano ya barabara ya Itigi hadi Tabora

Mvua yakata mawasiliano ya barabara ya Itigi hadi Tabora - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mvua yakata mawasiliano ya barabara ya Itigi hadi Tabora, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mvua yakata mawasiliano ya barabara ya Itigi hadi Tabora
kiungo : Mvua yakata mawasiliano ya barabara ya Itigi hadi Tabora

soma pia


Mvua yakata mawasiliano ya barabara ya Itigi hadi Tabora

Mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo katika eneo la Nyahua wilayani Uyui Mkoani Tabora imesababisha kukatika kwa barabara kuu ya Tabora kupitia Itigi hadi Dodoma na kusababisha magari ya abiria na mizigo kwishindwa kuendelea na safari zake kwa kutumia barabara hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika eneo la tukio Meneja wa Wakala wa Barabara )TANROADS) Mkoa wa Tabora  Mhandisi Damian Ndabalinze alisema mvua zilizonyesha katika maeneo hayo zimesababisha kukatika kwa eneo hilo ambapo ndipo barabara ya lami inaishia.

Aliwataka madereva wa magari ya aina yoyote kudiriki kupita katika aina hilo kwa sababu wanaweza kuhatarisha maisha yao na abiria na mizigo.

Ndabalinze alisema dereva yoyote atakayekaidi na kuamua kupita katika eneo hilo kwa kulazimisha jambo lolote litakalompata itakuwa ni yeye kajisababishia na asilelekeze lawama kwa chombo chochote.
  Baadhi ya wasafiri na wakazi wa Nyahua wilayani Uyui wakiwa katika eneo ambalo barabara imekatika kutoka na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha kukatika kwa mawasiliano baina ya Itigi na Tabora. Nyuma ni basi dogo la Prince  Ramigo linalofanya safari zake kutoka Tabora kwenda Dodoma kupitia Itigi.
Baadhi ya wasafiri kutoka katika Basi la Prince Ramigo na wakazi wa Nyahua wilayani Uyui wakijaribu kuvuka jana katika eneo ambalo barabara imekatika kutoka na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha kukatika kwa mawasiliano baina ya Itigi na Tabora. Nyuma ni basi dogo la Prince  Ramigo linalofanya safari zake kutoka Tabora kwenda Dodoma kupitia Itigi. 
  Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Tabora,  Mhandisi Damian Ndabalinze akizungumza na waandishi wa habari na wasafiri jana mara baada ya kutembelea eneo la tukio ili kujionea uharibifu wa barabara ulitokana na mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha kukatika kwa mawasiliano baina ya Itigi na Tabora
 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani Tabora SP Emilian  Kamuhanda akizungumza na waandishi wa habari na wasafiri jana mara baada ya kutembelea eneo la tukio ili kujionea uharibifu wa barabara ulitokana na mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha kukatika kwa mawasiliano baina ya Itigi na Tabora na kisha kutoa tahadhari kwa Madereva kutodiriki kupita katika eneo hilo.
  Basi la Prince Ramigo linalosafirisha abiria kutoka Dodoma kwenda Tabora likiwa limekwamwa katikati ya maji jana mara baada ya Dereva kujaribu kupita. Picha na Tiganya Vincent

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Mvua yakata mawasiliano ya barabara ya Itigi hadi Tabora

yaani makala yote Mvua yakata mawasiliano ya barabara ya Itigi hadi Tabora Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mvua yakata mawasiliano ya barabara ya Itigi hadi Tabora mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/mvua-yakata-mawasiliano-ya-barabara-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Mvua yakata mawasiliano ya barabara ya Itigi hadi Tabora"

Post a Comment