MCHEZAJI WA SIMBA ,TIMU YA TAIFA ARTHUR MAMBETA AFARIKI DUNIA

MCHEZAJI WA SIMBA ,TIMU YA TAIFA ARTHUR MAMBETA AFARIKI DUNIA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MCHEZAJI WA SIMBA ,TIMU YA TAIFA ARTHUR MAMBETA AFARIKI DUNIA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MCHEZAJI WA SIMBA ,TIMU YA TAIFA ARTHUR MAMBETA AFARIKI DUNIA
kiungo : MCHEZAJI WA SIMBA ,TIMU YA TAIFA ARTHUR MAMBETA AFARIKI DUNIA

soma pia


MCHEZAJI WA SIMBA ,TIMU YA TAIFA ARTHUR MAMBETA AFARIKI DUNIA

Na Zainabu Nyamka, Globu ya Jamii

MCHEZAJI wa zamani wa klabu ya Simba, Arthur Mambeta amefariki dunia  jana Alhamisi  baada ya kusumbuliwa na maradhi ya saratani kwa muda mrefu.

Mambeta aliyeanza kukipiga katika kikosi cha wanamsimbazi Simba SC mwaka 1960 ikiwa inaitwa   Sunderland akicheza nafasi kiungo mshambuliaji hodari kuanzia katika klabu yake hadi timu ya Taifa. 

Katika historia ya Arthur, aliyewahi kocha wa Tanzania miaka hiyo, Milan Celebic raia wa Yugoslavia alikaririwa akisema kuunda timu ya taifa bila ya Arthur Mambeta ni sawa na kula chakula bila ya chumvi au chai iliyokosa sukari.

 Arthur Mambeta ndiye mchezaji pekee wa Tanzania aliyekuwemo Katika kiķosi cha kwanza cha kombaini ya Afrika Mashariki iliyocheza na West Bromwich Albion ya England mwaka 1974 Uwanja wa Nakivubo mjini Kampala, Uganda.

Katika mechi hiyo ilijumuisha wachezaji wa timu ya mbalimbali kutoka  Afrika Mashariki akiwamo na mchezaji mwingine wa Tanzania aliyeteuliwa, Kitwana Manara alikuwa bechi kama kipa wa akiba kabla ya kuhamia kwenye ushambuliaji ambako pia alikuwa tishio hadi anastaafu soka.

Baada ya kustaafu soka, Mambeta alindelea kujihusisha na mchezo katika utawala na amewahi kuteuliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi Simba SC.

Hata hivyo, Mambeta alianza kujitoa taratibu kwenye soka baada ya kuanza kusumbuliwa na maradhi ya saratani yaliyosababisha akatwe miguu yake yote miwili. 

Taarifa zaidi kuhusu msiba huo na taratibu zake zinataolewa kutolewa na familia ya marehemu Alhamisi.

 Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Arthur Mambeta. Amin.


Hivyo makala MCHEZAJI WA SIMBA ,TIMU YA TAIFA ARTHUR MAMBETA AFARIKI DUNIA

yaani makala yote MCHEZAJI WA SIMBA ,TIMU YA TAIFA ARTHUR MAMBETA AFARIKI DUNIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MCHEZAJI WA SIMBA ,TIMU YA TAIFA ARTHUR MAMBETA AFARIKI DUNIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/mchezaji-wa-simba-timu-ya-taifa-arthur.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MCHEZAJI WA SIMBA ,TIMU YA TAIFA ARTHUR MAMBETA AFARIKI DUNIA"

Post a Comment