title : JUMIA TANZANIA YAAHIDI KUWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA, MAMILIONI YA WATEJA WALIOKO MTANDAONI
kiungo : JUMIA TANZANIA YAAHIDI KUWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA, MAMILIONI YA WATEJA WALIOKO MTANDAONI
JUMIA TANZANIA YAAHIDI KUWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA, MAMILIONI YA WATEJA WALIOKO MTANDAONI
KAMPUNI ya Jumia Tanzania inayojishughulisha na huduma za uuzaji na manunuzi ya bidhaa mbalimbali kwa njia mtandao imemtambulisha Zadok Prescott kuwa Mkurugenzi Mkuu wake mpya.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa utambulisho wake uliofanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo Prescott alibainisha ni fursa kwake kujiunga na kampuni hiyo.
Ambapo amesema Jumia ni kampuni ambayo imedhamiria kuleta mapinduzi ya biashara kwa njia ya mtandaoni hususani kwenye soko ambalo bidhaa zipo mbali na wateja pamoja na gharama kubwa za kufanya shughuli za masoko.
“Jumia ilianzishwa mnamo mwaka 2012 ikiwa na imani thabiti ya kwamba: ‘Mtandao wa intaneti unaweza kuboresha maisha ya Waafrika.’ "Ni vigumu kupata bidhaa unayoihitaji kupitia mfumo wa sasa wa manunuzi ya bidhaa mbalimbali Tanzania.
" Upatikanaji wa bidhaa katika sehemu tofauti huwalazimu wateja kusafiri umbali mrefu kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Kwa kuongezea, bei hutofautiana kwa kila mfanyabiashara jambo linalosababisha kuwa ni changamoto kutambua kama unauziwa bidhaa kwa bei sahihi au la,"amesema.
Ameongeza ni mfumo ambao humpotezea mteja muda na gharama katika maisha yake ya kila siku. Hivyo dhumuni kubwa la Jumia ni kuufanyia mabadiliko mfumo huo na kuufanya uwe wenye tija kwa wafanyabiashara nchini na kuwapatia wigo zaidi,” alisema Prescott.
Mkurugenzi Mkuu mpya wa KAMPUNI ya Jumia Tanzania,Zadok Prescott akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,alipokuwa akijitambulisha na kueleza mikakati mipya ya kuiendelea kampuni hiyo amayo kwa sasa imezidi kutanuka kila kukicha,kushoto kwake ni Meneja Masoko Albanny Jamess
Meneja Masoko wa Jumia Tanzania, Albanny Jamess akitoa ufafanuzi mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar,kuhusu ujio wa Mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo,na kuelezea namna Jumia ilivyodhamiria kuleta mapinduzi ya biashara kwa njia ya mtandaoni hususani kwenye soko ambalo bidhaa zipo mbali na wateja pamoja na gharama kubwa za kufanya shughuli za masoko.
Hivyo makala JUMIA TANZANIA YAAHIDI KUWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA, MAMILIONI YA WATEJA WALIOKO MTANDAONI
yaani makala yote JUMIA TANZANIA YAAHIDI KUWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA, MAMILIONI YA WATEJA WALIOKO MTANDAONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JUMIA TANZANIA YAAHIDI KUWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA, MAMILIONI YA WATEJA WALIOKO MTANDAONI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/jumia-tanzania-yaahidi-kuwakutanisha.html
0 Response to "JUMIA TANZANIA YAAHIDI KUWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA, MAMILIONI YA WATEJA WALIOKO MTANDAONI"
Post a Comment