title : MBUNGE HAWA MCHAFU AWAASA WANAJAMII KUJIEPUSHA NA VITENDO VIOVUhab
kiungo : MBUNGE HAWA MCHAFU AWAASA WANAJAMII KUJIEPUSHA NA VITENDO VIOVUhab
MBUNGE HAWA MCHAFU AWAASA WANAJAMII KUJIEPUSHA NA VITENDO VIOVUhab
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoani Pwani Hawa Mchafu amewataka wanajamii wote kudumisha amani na kujiepusha na vitendo viovu ikiwa ni pamoja na uhalifu, ubakaji, matumizi ya madawa ya kulevya, pombe haramu maarufu kama virobo na gongo,ukatili na ukandamizaji wa makundi mbalimbali katika jamii kama vile watoto, wanawake, wazee na wenye ulemavu.
Mchafu alisema hayo wakati wa siku ya kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani hapo jana yaliyofanyika katika kata ya Nyamato wilayani Mkuranga.
Mchafu aliongeza kwamba pamoja na unyanyasaji juhudi mbalimbali za wadau na serikali katika nchi yetu bado ukatili na unyanyasaji kwa wanawake ni mkubwa mno.”Katika wilaya yetu ya Mkuranga bado vitendo hivi vinaendelea katika baadhi ya maeneo ya kata na vijiji vyetu”. Mchafu alisema
Mchafu aliendelea kusema kwamba tayari serikali imechukua hatua mbalimbali ili kuondoa tofauti za kijinsia kwa kuingiza mitazamo ya kijinsia katika sera zinazowabagua wanawake “Nitumie fursa hii kuwaasa wanawake kujitokeza kushiriki katika fursa na nafasi mbalimbali na kufanya kazi kwa juhudi,maarifa na weledi mkubwa ili kufikia malengo ya Tanzania ya Viwanda.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu akipokea zawadi ya keki kutoka kwa Jukwaa la Wanawake Wila
ya ya Mkuranga.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu akipokea na kusoma mabango ya akina mama wa wilaya hiyo katika maadhimisho ya kilele cha siku ya Wanawake duniani yaliyofanyika Jana.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wilaya ya Mkuranga na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Mkuranga Mariam Ulega katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu akipokea mche wa Mkorosho baada ya kuzindua kitalu hicho katika maadhimisho ya kilele cha siku ya wanawake duniani jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Mkuranga Mariam Ulega.Picha na Emanuel Massaka.
Hivyo makala MBUNGE HAWA MCHAFU AWAASA WANAJAMII KUJIEPUSHA NA VITENDO VIOVUhab
yaani makala yote MBUNGE HAWA MCHAFU AWAASA WANAJAMII KUJIEPUSHA NA VITENDO VIOVUhab Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MBUNGE HAWA MCHAFU AWAASA WANAJAMII KUJIEPUSHA NA VITENDO VIOVUhab mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/mbunge-hawa-mchafu-awaasa-wanajamii.html
0 Response to "MBUNGE HAWA MCHAFU AWAASA WANAJAMII KUJIEPUSHA NA VITENDO VIOVUhab"
Post a Comment