title : MRADI WA MAJI WA BILIONI 4.9 WAENDELEA KUHUJUMIWA NAMTUMBO
kiungo : MRADI WA MAJI WA BILIONI 4.9 WAENDELEA KUHUJUMIWA NAMTUMBO
MRADI WA MAJI WA BILIONI 4.9 WAENDELEA KUHUJUMIWA NAMTUMBO
Na Yeremias Ngerangera, Namtumbo.
Mradi wa maji katika kijiji cha Likuyusekamaganga wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma umeingia dosari tena na kumfanya mkuu wa wilaya ya Namtumbo Sophia kizigo kuendesha zoezi la kupiga kura za siri ili kumbaini wanaohujumu mradi huo baada ya hivi karibuni vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 500 kuteketezwa kwa moto na tukio hilo kurudia tena siku ya jumatatano wiki hii na kuchoma mabomba ya mradi huo
Mwakilishi wa kampuni ya Elegance Developers Company Ltd ya Dar es salaam inayojenga mradi huo Mhandisi Felician Kavishe alisema vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 500 vilichomwa moto na watu wasiojulikana hivi karibuni lakini tukio hilo hilo limejirudia tena kwa kuchoma mabomba ya kusambazia maji ambayo thamani yake bado haijajulikana.
Aidha kavishe alionesha wasiwasi wake kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo kuendelea kutekeleza mradi huo katika mazingira ya hofu zilizojaa mioyoni mwao juu ya matukio ya mara kwa mara ya kuchoma vifaa na mwisho wa yote akadai isije wakachomwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Kaimu Mtendaji wa kata ya Likuyuseka Petro Nyoni alidai kitendo cha mkuu wa wilaya hiyo kuendesha zoezi la kupiga kura za siri kwa wananchi wa kijiji hicho linaweza kuwa suluhisho la kumalizika kwa tatizo hilo kutokana na wananchi hao kuwajua watu wanaofanya hujuma hiyo kwa kuwapigia kura za siri za ushindi .
Mkuu wa wilaya hiyo aliwaambia wazee wa kijiji hicho kuwa serikali imeleta bilioni 4.9 kutatua changamoto ya maji na kuelekeza lawama zake kwa wazee wa kijiji hicho kwa kulifumbia macho tatizo hilo la uchomaji moto wa vifaa vya mradi vinavyoletwa na mkandarasi huku wa zee hao wakibaki kimya alisema mkuu wa wilaya hiyo.
“Wazee huo ni ujinga kuendelea kuacha kudhibiti tatizo hili ambalo mliweza kulitatua wazee wa kijiji hiki lakini mkaendelea kubaki kimya na matukio yanaendelea kutokea huku wazee wa kijiji mpo” alisema Mkuu wa wilaya hiyo.
Hata hivyo mkuu wa wilaya aliendesha zoezi la kupiga kura za siri kwa wananchi wa kijiji hicho kuwataja watu wanaojihusisha na matukio ya uchomaji moto vifaa vya mradi huku matokeo ya kura hizo zikabaki kuwa siri kwa hatua za uchunguzi zaidi.
Mhandisi mshauri Nashoni Charles kutoka kampuni ya Norplan Tanzania Ltd ya Dar es salaam alisema kitendo cha kuendelea kuchoma vifaa kinaiingizia hasara kampuni lakini pia kitafanya kampuni hiyo kutumia muda mwingine kwenda kununua vifaa , huku muda wa mkataba wa utekelezaji wa mradi huo upo palepale.
Kwa mujibu wa mhandisi mshauri wa kampuni hiyo Nashon alidai mradi huo wa maji wa Likuyumandela umefikia asilimia 60 kwa sasa katika utekelezaji wake na unategemea kuhudumia watu 13,319 kwa kipindi cha miaka kumi baada ya kukamilika kwake.
Kaimu Mhandisi wa maji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Salumu Nachundu alidai mradi unatekelezwa chini ya progamu ya maendeleo ya sekta ya maji (WSDP)kupitia program ndogo ya maji na usafi wa mazingira vijijini (RWSSP)
Hivyo makala MRADI WA MAJI WA BILIONI 4.9 WAENDELEA KUHUJUMIWA NAMTUMBO
yaani makala yote MRADI WA MAJI WA BILIONI 4.9 WAENDELEA KUHUJUMIWA NAMTUMBO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MRADI WA MAJI WA BILIONI 4.9 WAENDELEA KUHUJUMIWA NAMTUMBO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/mradi-wa-maji-wa-bilioni-49-waendelea.html
0 Response to "MRADI WA MAJI WA BILIONI 4.9 WAENDELEA KUHUJUMIWA NAMTUMBO"
Post a Comment