title : MAWAZIRI WA AFYA KUTOKA NCHI 10 WAJADILIANA NAMNA YA KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA AFYA
kiungo : MAWAZIRI WA AFYA KUTOKA NCHI 10 WAJADILIANA NAMNA YA KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA AFYA
MAWAZIRI WA AFYA KUTOKA NCHI 10 WAJADILIANA NAMNA YA KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA AFYA
Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii
MAWAZIRI wa Afya kutoka nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini wamekutana nchini Tanzania kwa ajili ya kujadili namna ya kuboresha huduma za afya na hasa katika utambuzi na kubaini magonjwa ya mlipuko.
Pia mawaziri hao wamekutana kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika utoaji na usimamizi bora wa huduma za afya.Mbali ya mawaziri pia wadau wa sekta ya afya kutoka kwenye baadhi ya mashirika wameshiriki mkutano huo.
Kupitia mkutano huo wa afya wa 65 nchi zisizo na uzoefu zitajifunza kutoka nchi ambazo zinafanya vizuri katika utoaji huduma,usimamizi na kutathimi ambapo washiriki wakiwamo mawaziri wa afya pamoja na wadau wa afya wameendelea kubadilisha uzoefu kupitia mada mbalimbali zinazoendelea kutolewa na watoa mada.
Kwa Tanzania, mwenyeji wa mkutano huo ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ni miongoni mwa wanaoshiriki mkutano huo unaojadili masuala ya afya kwa nchi hizo.
Kauli mbiu katika mkutano huo inasema "Ushirikiano wa sekta ya afya katika kupata mafanikio ya malengo ya maendeleo endelevu(SDG's)" na mkutano huo huo utakaofanyika kwa siku tatu inasema hivi.
Hivyo nchi mbalimbali wameelezea namna ambavyo wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali katika sekta ya afya.Mwakilishi kutoka nchi ya Uganda pamoja na kuelezea ambavyo wamefanikiwa katika sekta ya afya lakini changamoto kubwa ipo katika ajali za barabarani ambazo nyingi zinatokana na uendeshaji usifuata sheria unaofanywa na waendesha pikipiki.
Akizungumza kwenye mkutano huo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema nchini Tanzania kuna mikakati mbalimbali ya kuboresha huduma za afya.Pia ameelezea hivi karibuni watazindua chanjo ya kansa kwa msichana wa kike kuanzia miaka 9 hadi miaka 13.
Amesema lengo ni kukabiliana na tatizo la ugonjwa wa kansa na lengo la Serikali ni kuhakikisha ugonjwa wa kansa unapungua.Wakati wa mkutano huo pia wamejadili sera mbalimbali kwa kila ambazo zipo kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya.
Hivyo makala MAWAZIRI WA AFYA KUTOKA NCHI 10 WAJADILIANA NAMNA YA KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA AFYA
yaani makala yote MAWAZIRI WA AFYA KUTOKA NCHI 10 WAJADILIANA NAMNA YA KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA AFYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAWAZIRI WA AFYA KUTOKA NCHI 10 WAJADILIANA NAMNA YA KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA AFYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/mawaziri-wa-afya-kutoka-nchi-10.html
0 Response to "MAWAZIRI WA AFYA KUTOKA NCHI 10 WAJADILIANA NAMNA YA KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA AFYA"
Post a Comment