JHIKOMAN, CHUO CHA TaSUBa WAZINDUA RASMI ALBAM YA SAFARI YA GITAA BARIDI

JHIKOMAN, CHUO CHA TaSUBa WAZINDUA RASMI ALBAM YA SAFARI YA GITAA BARIDI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa JHIKOMAN, CHUO CHA TaSUBa WAZINDUA RASMI ALBAM YA SAFARI YA GITAA BARIDI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : JHIKOMAN, CHUO CHA TaSUBa WAZINDUA RASMI ALBAM YA SAFARI YA GITAA BARIDI
kiungo : JHIKOMAN, CHUO CHA TaSUBa WAZINDUA RASMI ALBAM YA SAFARI YA GITAA BARIDI

soma pia


JHIKOMAN, CHUO CHA TaSUBa WAZINDUA RASMI ALBAM YA SAFARI YA GITAA BARIDI

Na Andrew Chale, BAGAMOYO 

MWANAMUZIKI nguli wa miondoko ya Afro reggae, Jhikolabwino Manyika maarufu Jhikoman kwa kushirikiana na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Ijumaa ya 14 Desemba, 2018, amezindua rasmi albam yenye nyimbo sita tukio lililofanyika mjini Bagamoyo,Mkoani Pwani.

Jhikoman ambaye anatoka kwenye lebo ya AfriKabisa ameweza kuonesha ukongwe katika muziki huo kwa kufanya kazi pamoja na vijana wadogo ambao ni wanafunzi wa Chuo cha Sanaa TaSUBa na kukonga nyoyo mashabiki waliojitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi huo.

Albam hiyo ina beba nyimbo kama: Mara ya kwanza, Ndotoni, Safari, Bad mind,Time to love na Kuagana zilizo kwenye mtindo wa regge.

Katika uzinduzi huo, Msanii Vitalisi Maembe na wengine wakiwemo Sinaubi Zawose, Voice of Revolution, K’Gwana Shija pamoja na Bocka T waliwez kupamba jukwaa katika kusindikiza uzinduzi huo kwa kuimba nyimbo zao mbalimbali.

Jhikoman ameshukuru uongozi wa TaSUBa kwa ushirikiano wa kutayarisha albam na kuirekodi kupitia studio ya chuo hicho.

“Wasanii waliopiga vyombo na kuimba na mimi hapa jukwaani ndio nilioshirikiana nao katika albam hii ni wa TaSUBa. Nashukuru kwa Uongozi kuwapa fursa ya kufanya kazi hii. Lakini pia nawashukuru Watanzania kuendelea kutuunga mkoni katika kazi zetu na kwa sasa albam itakuwa inapatikana pale Afrikakabisa hapa Bagamoyo na maeneo mengine tutaendelea kuwatangazia” alieleza Jhikoman.


Msanii Jhikoman wa Afrikabisa akishirikiana na Wanafunzi wa TaSUBa wakiimba baadhi ya nyimbo zilizopo kwenye albam ndogo ya Safari ya Gitaa Baridi iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa TaSUBa na Afrikabisa wakati wa uzinduzi huo Usiku wa Ijumaa ya 14 Desemba 2018. 




Hivyo makala JHIKOMAN, CHUO CHA TaSUBa WAZINDUA RASMI ALBAM YA SAFARI YA GITAA BARIDI

yaani makala yote JHIKOMAN, CHUO CHA TaSUBa WAZINDUA RASMI ALBAM YA SAFARI YA GITAA BARIDI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala JHIKOMAN, CHUO CHA TaSUBa WAZINDUA RASMI ALBAM YA SAFARI YA GITAA BARIDI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/jhikoman-chuo-cha-tasuba-wazindua-rasmi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "JHIKOMAN, CHUO CHA TaSUBa WAZINDUA RASMI ALBAM YA SAFARI YA GITAA BARIDI"

Post a Comment