title : Manispaa ya Ilala yapitisha bajeti ya sh. bilioni 287
kiungo : Manispaa ya Ilala yapitisha bajeti ya sh. bilioni 287
Manispaa ya Ilala yapitisha bajeti ya sh. bilioni 287
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
BARAZA la Madiwani Manispaa ya Ilala imepitisha bajeti ya sh.bilioni 287 katika mwaka fedha wa 2018/2019 ikilinganishwa bajeti iliyopita ya 2017,2018 ya sh.bilioni 124.
Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Mchumi wa Manispaa hiyo, Ando Mwanduga amesema kuwa bajeti hiyo katika sehemu kubwa ni kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
Mwanduga amesema kuwa fedha hizo zitapatikana katika makundi mawili ya ruzuku pamoja na vyanzo vya ndani ambapo hakuna mwananchi atakayeonewa katika bajeti hiyo.
Amesema kuwa chanzo cha mapato ya ndani ni wanatarajia kukusanya sh.bilioni 56.8 ambapo na fedha nyingine zitakuwa ni za ruzuku.Mwanduga amesema kuwa kila diwani anataka kuwa na mradi katika kata yake lakini haiwezikani kutokana na uwezo wa manispaa.
Amesema kuwa bajeti hiyo itatekelezeka ni pamoja na kuwa na vyanzo hivyo viwili vya ruzuku na mapato ya ndani na asilimia 60 ni kwa ajili ya maendeleo ya wananchi katika kutekeleza miradi.
Aidha amesema kuwa kutokana na serikali ya awamu ya tano ya elimu bure kwa manispaa imethubu ikiwa ni pamoja na kujenga shule nne pamoja na kufanya ukarabati kwa bajeti iliyoishia 2018.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akizungumza wakati wa Kikao cha Bajeti cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Anatoglo
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala,Ando Mwankuga akiwaeleza Madiwani jinsi mipango na miradi ya Maendeleo katika kata ya Segera itakavyoendeshwa.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala ,Omary Kumbilamoto akiwasilisha makadilio ya bajeti ya Mwaka 2018/ 2019.
Wabunge wa jimbo la Ilala na Segerea , Azzan Zungu na Bonnah Kaluwa wakisoma kwa makini makblasha ya bajeti ya Manispaa ya Ilala.
Hivyo makala Manispaa ya Ilala yapitisha bajeti ya sh. bilioni 287
yaani makala yote Manispaa ya Ilala yapitisha bajeti ya sh. bilioni 287 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Manispaa ya Ilala yapitisha bajeti ya sh. bilioni 287 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/manispaa-ya-ilala-yapitisha-bajeti-ya.html
0 Response to "Manispaa ya Ilala yapitisha bajeti ya sh. bilioni 287"
Post a Comment